Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani
Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the love

MADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yalivyo wafumbua macho na kuwafanya kufahamu sheria mbalimbali za barabarani na hivyo kuendelea na kazi yao wakiwa salama. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wamesema hayo mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wametembelea kijiwe cha bodaboda cha Kijiwe Pesa ambapo baadhi ya bodaboda walikuwa wakifanya tathmini kuhusu mafunzo waliyopata kutoka Amend kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi ambao wameendelea kufanikisha kutolewa kwa mafunzo hayo.

Madereva hao bodaboda katika kijiwe hicho wamesema awali hawakuwa wakifahamu vema sheria za usalama barabarani hasa taa zinazoongoza magari na jinsi ya kupita kwenye makutano ya barabara ilikuwa ni kitendawili kwao.

“Kupitia mafunzo ya usalama barabarani ambayo tumeyapata kutoka kwa wenzetu wa Amend kwa kushirikiana na wadau wengine kama Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani sasa tunafahamu vema sheria za usalama barabarani pamoja na alama zilizopo,” amesema dereva bodaboda Jonathan Chidawi

Kwa upande wake Amiri Matimba ambaye ni  Msaidizi wa Miradi kutoka Shirika la Amend Tanzania anasema wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa madereva bodaboda 47 kwa wiki ya kwanza jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa  wanaendelea kutembea katika vijiwe mbalimbali vya bodaboda kwa ajili ya kuhamasisha maofisa hao kusafirishaji(bodaboda)kujiunga katika mafunzo hayo yanayotolewa bila gharama yoyote.

Wakati huo huo Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambae pia ni Katibu wa Chama cha Walimu wa madereva Tanzania (CHAWATA) Massava Ponera akieleza tathimi ya mafunzo hayo toka walipoanza hadi walipofikia amesema mafunzo yanaendelea na madereva wengi wamefikiwa na mafunzo hayo.

Amefafanua kwa Dodoma hiyo ni awamu ya pili kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yamedhaminiwa na ubalozi wa Uswisi ili kuwezesha elimu ya usalama barabarani inafika kwa kundi la bodaboda ambalo jamii siku zote hulitazama kwa jicho la tofauti na kuamini ni wavunjaji wa sheria wakubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!