Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makamba ataja maeneo ya kuboresha mambo ya nje
Habari za Siasa

Makamba ataja maeneo ya kuboresha mambo ya nje

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba
Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ametumia takribani saa moja kuelezea maeneo ambayo yatajajadiliwa katika warsha ya Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani inayofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Kibaha kuanzia tarehe 21 hadi 24 Aprili 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Makamba amewataka washiriki wa warsha hiyo ambao ni Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Mabalozi, Wakuu wa Utawala balozini, Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa Wizara hiyo kujadili kwa upana maeneo hayo ili Wizara iweze kufikia malengo iliyowekewa na Serikali.

Maeneo ambayo ameyataja, Waziri Makamba ni pamoja na kuboresha mawasiliano ndani ya Wizara, baina ya Wizara na taasisi nyingine na wadau wake. Amesema hakuna namna Wizara ambayo majukumu yake ni uratibu ikafikia ufanisi unaohitajika bila kuwa na mfumo madhubuti wa mawasiliano.

Amesema eneo lingine ni umuhimu wa Wizara kuweka mfumo madhubuti zaidi wa kufuatilia utekelezaji wa matukio ambayo imekuwa ikiyaratibu tena kwa ufanisi mkubwa. Matukio hayo ni pamoja na masuala yanayoafikiwa katika ziara za viongozi, Mikutano, makongamano ambayo yana faida kubwa kwa nchi kama yatafuatiliwa vyema utekelezaji wake.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu wa Wizara wa kuweka mfumo wa kuwaongezea maarifa, weledi na ujuzi maafisa wake, hususan katika uandishi na kuzungumza.

Amebainisha kuwa nchi yetu inasifika na kutangazika kutokana umahiri wa wanadiplomasia wake, jambo ambalo limekuwa ni kama urithi wetu, hivyo lazima jambo hili liendelezwe kwa kuwapatia watumishi ujuzi unaohitajika.

Pia amesisitiza ni umuhimu wa kuwa na mfumo wa kuwajibishana. Amesema mfumo huo utasaidia kuhamasisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika Wizara.

Alisisitiza pia umuhimu wa kuendelea kulinda heshima na hadhi ya nchi yetu huko Nje. Alisema kuwa kufanikisha hilo ni pamoja na kuwa na mazingira bora ya utendaji kazi huko nje ikiwa ni pamoja na kuwa na vitendea kazi vinavyohitajika.

Alisema Serikali itahakikisha inaboresha mazingira ya kazi ili nchi iendelee kulinda heshima yake iliyojengwa kwa muda mrefu na viongozi waliopita.

Makamba alihitimisha mazurngumzo yake kwa kuwapongeza Mabalozi kwa kazi nzuri wanayofanya licha ya changamoto wanazokabiliana nazo. Amesema tokea ateuliwe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa muda wa miezi saba sasa amebaini kuna uwezekano wa kufanya mambo makubwa zaidi na ndiyo moja ya sababu ya kuitisha warsha hiyo ambayo ameitaja kuwa ni ya kubainisha changamoto, kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mpango wa utekelezaji wenye tija kwa maslahi ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!