Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni
Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene
Spread the love

 

WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake ya kiasi cha Sh. 1.1 trilioni, kwa mwaka wa fedha wa 2024/25. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha, leo Ijumaa, bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, ametoa mchanganuo wa bajeti hiyo akisema Sh. 922.75 bilioni zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 178.3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa bungeni na Simbachawene alichangua bajeti za mafungu ya taasisi zilizoko chini ya wizara yake, ambapo ofisi ya Rais Ikulu ambayo ni fungu namba 20, imeongezeka kutoka Sh. 32.15 bilioni iliyoidhinishwa 2023/24, hadi kufikia Sh. 33.5 inayoombwa katika mwaka wa fedha wa 2024/25.

Simbachawene amesema, Ofisi ya Rais Ikulu na taasisi zake ikiwemo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Taasisi ya Uongozi, TASAF, Wakala wa Ndege za Serikali na Mamlaka ya Serikali mandao, katika 2024/25 imepanga kutumia Sh. 33.5 bilioni.

Hali kadhalika, bajeti ya Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri imeongezeka kutoka Sh. 860 bilioni ilizoidhinishiwa 2023/24, hadi kufikia Sh. 969.2 bilioni, inayoombwa kwa 2024/25.

Waziri huyo amesema, Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri ambayo fungu lake ni namba 30, imepanga kutumia Sh. 805.6 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 110 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!