Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaunda kamati kuchunguza mauaji hifadhini Serengeti, Tarime
Habari za Siasa

Serikali yaunda kamati kuchunguza mauaji hifadhini Serengeti, Tarime

Spread the love

SERIKALI imeunda kamati ya kitaifa kwenda kushughulikia mauaji ya raia yanayodaiwa kufanyika katika maeneo ya Hifadhi ya Serengeti, mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebanishwa jana Jumapili na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana, katika kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya chama hicho wilayani Serengeti mkoani Mara.

Ni baada ya baadhi ya wajumbe kuiomba serikali kuingilia kati ili mauaji hayo yakomeshwe kwa kuwa yanaichafua nchi.

“Lakini niwape taarifa nyingine, baada ya haya mambo mbalimbali yanayotokea karibuni huku Serengeti na Tarime maeneo ya hifadhini. Kuna kamati ndogo itakuja kitaifa kupitia maeneo yote haya na kuangalia juu ya tatizo hili na mauaji yanaenda kushughulikiwa,” alisema Kinana.

Kinana alisema Serikali hairuhusu raia kukatisha uhai wake kwa kuwa ni kinyume na katiba ya nchi, hivyo kama mtu atafanya kosa anatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria na sio kuuliwa.

“Serikali hairuhusu raia yoyote maisha yake yasitishwe kwa sababu yoyote ile, vyombo vya sheria, ulinzi na usalama kazi yake mtu akikosea kukamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya kisheria,” alisema Kinana.

“Tatizo hili huwezi kulaumu upande mmoja peke yake, sisi kama CCM kama serikali tunawajibu kuwaelimisha wananchi kuheshimu mipaka ya hifadhi. Jambo la msingi hakuna mtu ana haki kuondoa maisha yamtu, kumpiga mtu risasi kumuuwa kwenye katiba ya nchi haipo, haki ya kwanza ya msingi kuishi,” alisema Kinana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!