Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi Kapele-Ndalambo warahisishiwa kufika Tunduma
Habari Mchanganyiko

Wananchi Kapele-Ndalambo warahisishiwa kufika Tunduma

Spread the love

Ukarabati wa barabara ya Kakozi – Ilonga yenye urefu wa kilomita 49.6 umeelezwa kuondoa adha kwa wananchi wa kata ya Kapele na Ndalambo wilayani Momba mkoani Songwe waliokuwa wakitumia siku saba kufika Tunduma. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).

Ukarabati kwa barabara hiyo umekuja baada ya kupandishwa hadhi na kusimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) mkoa wa Songwe kutoka Wakala wa barabara za mijini na vijijini (Tarura).

Wakizungumza na MwanaHALISI Online kwa nyakati tofauti leo Jumatano baadhi ya wananchi  wamesema barabara hiyo ilikuwa kikwazo kwao kiuchumi lakini kwa sasa imekuwa chachu ya maendeleo kwani inawafikisha maeneo muhimu ikiwemo mji wa Tunduma.

Mkazi wa kijiji cha Kakozi, Godi Mtambo amesema ubovu wa barabara hiyo ulikuwa ukiwasababisha magari kukwama njiani pindi wanapoenda Tunduma kusaka mahitaji muhimu.

“Barabara hii imekuwa mkombozi, wakulima wengi wa Kata za Kapele na Ndalambo wameanza kunufaika  kwa kusafirisha mazao,” amesema.

Naye Agnesi Sichalwe amesema wafanyabiashara walikuwa wanashindwa kufika kununua mazao wakihofia kukwama kwa magari yao hali ambayo iliyosababisha uchumi wa wananchi kushuka.

Mtendaji wa kijiji cha Kakozi, Maria Maketta amesema kuboreshwa kwa barabara hiyo kutafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Sumbawanga vijijini na nchi jirani ya Zambia kupitia Wilaya ya Momba.

Diwani wa Kata ya Ndalambo, Fravian Sichizya amesema awali barabara hiyo ilikuwa inasimamiwa Tarura lakini kwa sasa imepandishwa hadhi na kusimamiwa na Tanroad Mkoa wa Songwe ambao wameanza  mchakato wa kuboresha.

“Serikali inatakiwa kuiweka kwenye bajeti barabara hiyo ili ijengwe kwa kiwango cha lami,” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala Barabara Tanzania Mkoa wa Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga amesema kabla ya kupandishwa hadhi barabara hiyo, wananchi walikuwa wanashindwa kusafirisha mazao kutoka nchi jirani ya Zambia kuelekea eneo la Kasesa kutokea maeneo ya wilaya ya Momba na Rukwa wilaya ya Sumbawanga vijijini.

“Licha ya kukarabati barabara hiyo bado kuna maeneo korofi ambayo kwa sasa wakandarasi wapo eneo la kazi kurekebisha na kuhakikisha yanapitika,” amesema mhandisi Bishanga.

Katika hatua nyingine Mhandisi Bishanga amesema Tanroad mkoa wa Songwe katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan wametumia zaidi ya Sh. 170 bilioni katika matengenezo ya barabara kuu, mkoa na madaraja likiwepo daraja la mto Momba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!