Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango atishia kujiuzulu
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango atishia kujiuzulu

Spread the love

MAKAMU wa Rais, Dk. Phillip Mpango ametishia kujiuzulu endapo Wizara ya Maji, itashindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro, uliokwama kwa takribani miaka 10. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Mpango ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, alipofanya ziara ya kushtukiza kuutembelea mradi huo wa Maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambapo ameagiza hadi kufika Juni 2024 uwe umeshakamilika.

Mradi wa maji wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

“Ninataka kuona mradi huu unafanya kazi ifikapo Juni 2024 maji yatoke Same na Mwanga, mjipange vizuri na msimamie wakandarasi usiku na mchana maji yatoke mradi usipotoa maji nitaacha kazi, na nikiacha kazi Katibu Mkuu na watu wake sijui itakuwaje,” amesema Dk. Mpango na kuongeza:

“Hatuwezi kurudi na kuja kuwaangalia wananchi na kuwaambia wasubiri, maji haya ni rasilimali kubwa na bila maji hakuna uhai, mazingira yatunzwe ili kulinda vyanzo vya maji.”

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, akitoa taarifa ya mradi huo, alisema ujenzi wake umefikia asilimia 85.7 na kwamba watajitahidi kutimiza agizo la Dk. Mpango.

Mradi huo unalenga kutatua kero ya uhaba wa maji safi na salama katika miji ya Wilaya za Same na Mwanga, mkoani Kilimanjaro na vijiji vitano wilayani Korogwe, Mkoa wa Tanga. Unatarajiwa kunufaisha wananchi 438,000.

Mradi huo kwa sasa unatekelezwa chini ya Kampuni ya M.A Kharif & Sons, ambapo Machi 2023 ilisaini makubaliano ya kuhuisha mkataba na Wizara ya Maji, baada ya kuuvunja mkataba wa awali 2020 kwa makosa ya kugushi nyaraka muhimu za kimkataba na kujipatia fedha kwa njia ya udanfanyifu.

Mradi huo unajengwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo, Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Uchumi wa Afrika (BADEA) na Shirikisho la Nchi Wanachama Wauzaji wa Mafuta ya Petroli (OPEC).

Mikataba ya utekelezwaji wa awamu ya kwanza ya mradi uliopangwa kutumia Dola za Marekani 112.69 milioni,  ilianza kusainiwa Novemba 2014 kati ya Serikali na  Mkandarasi M.A Kharafi & Sons, hadi  Oktoba 2016 ulipochukuliwa na mkandarasi Badr East Africa Enterprises Ltd.

Mradi huo ulitarajiwa kukamilika tarehe 16 Julai 2017, kwa ujenzi wa chanzo cha maji, chujio, tenki la kuhifadhi maji Kisangara na ujenzi wa bomba la kusafirisha maji ghafi kwenda kwenye chujio na ujenzi wa bomba la kusafirisha maji yaliyotibiwa kwenye tenki la Kisangara.

Mikataba ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi ilisainiwa Agosti 2018 kati ya Serikali na mkandarasi Badr East Afriva Enterprises ltd wenye thamani ya Dola za Marekani 36.0 milioni na ulitarajiwa kukamilika Machi 2021, hata hivyo mkataba ulitishwa Desemba 2020.

2 Comments

  • Hongera mpango mzee umebaki pekee yako mwadilifu… Wengine akili zao zipo tu kwenye Mpira wanatoa pesa kwenye Mpira kumbe Kuna watu hata maji hawana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

error: Content is protected !!