SERIKALI imetakiwa kuhakikisha magari ya viongozi wa umma wakiwemo mawaziri, yanabadilishwa mfumo wa matumizi ya mafuta kwenda gesi ili kubana matumizi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Wito huo umetolewa leo tarehe 15 Machi 2024 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ilipotembelea vituo vya kujazia gesi vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Mathayo, amesema gharama za gesi ni nafuu ikilinganishwa na mafuta ya dizeli na petroli, hivyo serikali inapaswa kuhakikisha magari ya viongozi yakayonunuliwa yanakuwa na mifumo ya moja kwa moja ya matumizi ya nishati hiyo.
“Kama mlivyosikia gharama ya gesi iko chini ukilinganisha kama mafuta ya kwaida ya dizeli na petrol na unakwenda umbali mrefu. Tunapenda kuwashauri TPDC na serikali kuwe na vituo vya kutosha. Tunashauri serikali na wauza magari wauze ambayo tayari yameshatengenezwa kw amfumo wa kutumia gesi hata magari ya serikali yanayoingia baadae yajipange yawe na mifumo ya gesi,” amesema Mathayo.
Katika hatua nyingine, Mathayo ameitaka Serikali kupunguza kodi katika vifaa vya kuweka mifumo ya gesi katika magari ili kupunguza gharama kwa lengo la kuvutiwa wananchi wengi kutumia gesi kwa gharama nafuu.
Pia, Mathayo ameishauri Serikali kuongeza idadi ya vituo vya kujaza gesi katika magari na karakana za kubadilisha mifumo.
Akijibu mapendekezo hayo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu.
Amesema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeandaa mkakati wa kuongeza vituo vya kujazia gesi kutoka idadi ya vitano iliyopo sasa hadi kufikia 15.

Leave a comment