Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Paroko amshukia diwani, mbunge Ulanga
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Paroko amshukia diwani, mbunge Ulanga

Spread the love

PAROKO wa Kanisa Katoliki la Sali, Padri Charles Kuandika, amemshukia Mbunge wa Ulanga Mashariki, Salim Almasi (CCM) na Diwani wa Kata ya Sali, Tarsis Noya, mkoani Morogoro kwamba kama kazi ya kuwawakilisha wananchi imewashinda, bora waachie ngazi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbunge wa Ulanga Mashariki, Salim Almasi

Padri Kuandika ametoa kauli hiyo hivi karibuni kufuatia kukatika kwa mawasiliano kati ya kijiji hicho na makao makuu ya wilaya ya Ulanga huku mbunge na diwani wake wakishindwa kuchukua hatua wala kufika kushuhudia kiwango cha uharibifu.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sali wakifanya matengenezo ya barabara ya kijiji hicho baada ya kuhimizwa.

Alizungumza wakati wa misa ya mazishi ya Mzee Ambrose Mtendagi, Padri Kuandika alisema barabara ya Sali imekatika kiasi kwamba kama kuna mgonjwa anahitaji  kukimbizwa katika hospitali ya wilaya Ulanga, hawezi kufika kwa sababu haipitiki kwa gari wala pikipiki.

“Nimeangalia umati wa watu waliofika hapa kijijini Sali kwa ajili ya msiba huu, nikajiuliza wamefikaje hapa na watafikaje kwao maana barabara ni mbovu sana,  haipitiki. Nikajiuliza viongozi wetu yaani mbunge na diwani wako wapi? ‘ alihoji Padri Kuandika.

Alisema hana maana kwamba mbunge na diwani watoe fedha zao mfukoni, la hasha bali uwepo wao na sauti zao kwenye vyombo wanavyowakilisha, zingesaidia kukabiliana na changamoto za kijiji hicho.

Paroko huyo alielekeza masikitiko yake kwa Mbunge wa Ulanga, Salim kuwa tangu alipochaguliwa hadi leo hajafika kijijini hapo kuzungumza wananchi wake.

“Sijamwona mbunge wala diwani tangu walipochaguliwa. Mimi naomba wafikishieni salaam, kama kazi walizoomba zimewashinda, bora wang’atuke. Sali ina changamoto nyingi kwanini viongozi wetu hawataki kufika kushuhudia matatizo ya wananchi wao,” alihoji

Paroko huyo ambaye pia ni mlezi wa Seminari ndogo ya Kasita ya Sali, aliwahamasisha wananchi kujitolea nguvu kazi zao kwa ajili ya kurekebisha barabara hiyo.

” Nitasimamisha masomo ya vijana wangu kwa siku moja, tuungane na wananchi wote kwenda kufanya marekebisho ya barabara hiyo ili iweze kupitika,” alisema.

Tayari kazi ya kurekebisha barabara hiyo kwa kutumia  nguvu za kazi  ya wananchi imeanza baada ya paroko huyo kuhamasisha wananchi kujitolea.

1 Comment

  • Hongera baba Paroko. Umetumia akili nyingi sana. Mwenyezi Mungu uzidi kutubariki na kututunza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

error: Content is protected !!