Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mama (53) atolewa ganda la pipi kwenye pafu, aliishi nalo miaka 11
Habari Mchanganyiko

Mama (53) atolewa ganda la pipi kwenye pafu, aliishi nalo miaka 11

Spread the love

Watalaam wa Magonjwa ya Mfumo wa Mapafu na Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, leo Jumatatu wamemtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi lilipo na kulinasa na kisha kulitoa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

 Akizungumza baada ya kutoa ganda hilo, Daktari wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dk. Hedwiga Swai amesema mgonjwa huyo alikuja akiwa na tatizo la mapafu yake kuharibika na kutoa usaha vilevile alikua anatoa makohozi yenya harufu kali.

“Mgonjwa huyo alikuja kwa lengo la kufanya vipimo vya kifua (Bronchoscopy) ila baada ya kuingiza kifaa chenye kamera kwenye mapafu tuliona kuna kitu ambacho sio cha kawaida katika pafu lake la kushoto na tulipoangalia vizuri tuligundua kuwa huo haukua uvimbe bali ni ganda la plastiki” amesema Dk. Swai.

Dk. Swai ameeleza kuwa mgonjwa huyo alikua anamng’unya pipi na ganda lake mwaka 2013 kwa bahati mbaya akameza na ganda lake na alipoenda hospitali hawakuona tatizo lolote na baada ya muda alianza kukohoa na kutoa usaha, ndipo alipoanza kutumia dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu bila mafanikio yoyote.

Dk. Swai ameitaka jamii kuacha tabia ya kuchezea vitu mdomoni ambavyo vinaweza kuleta madhara kwakuwa kitu hicho kikingia kwenye mfumo wa hewa kinaweza kusababisha madhara mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!