Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yamjibu Makonda
Habari za Siasa

Chadema yamjibu Makonda

John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiko tayari kufanya mdahalo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, endapo Serikali itafanyia kazi madai yao juu ya upatikanaji tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam..(endelea).

Msimamo huo umetolewa leo tarehe 15 Januari 2022 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema,  John Mrema siku moja  baada ya Makonda kutaka mdahalo na viongozi wa chama hicho.

“Msimamo wa chama ni kuwa, kama anataka mdahalo na sisi kama chama tupo tayari na hatujawahi kukimbia midahalo kama wao na chama chao. Hivyo basi, mdahalo unaweza kufanyika katika masuala yafuatayo ambayo tumeweka msimamo wetu wazi ili yatekelezwe na Serikali,” imesema taarifa ya Mrema.

Taarifa ya Mrema imetaja mambo hayo kuwa ni Serikali kuondoa bungeni miswada mitatu ya marekebisho ya sheria za uchaguzi ambayo Chadema inadai kuwa mibovu. Serikali ianzishe mara moja mchakato wa marekebisho ya katiba ya 1977 ili kuwezesha kuondoa mapungufu yaliyopo kwenye katiba hiyo ili kuruhusu maandalizi ya kuandikwa miswada mipya ya kuboresha mifumo ya ucvhaguzi.

Aidha, kupitia taarifa hiyo Mrema amesema mpango wa Chadema kufanya maandamano yasiyo na kikomo kuanzia tarehe 24 Januari mwaka huu, hadi Serikali itakapofanyia kazi madai yao, uko palepale.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!