Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Silaa asimamisha matumizi ya kituo cha mafuta cha Barrel Dar
Habari MchanganyikoTangulizi

Silaa asimamisha matumizi ya kituo cha mafuta cha Barrel Dar

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa
Spread the love

 

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni jijini Dar es salaam na kupiga marufuku ujenzi holela wa vituo vya mafuta nchi nzima vinavyojengwa kwenye makazi ya watu hatua inayohatarisha usalama wa watu na mali zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Silaa ametoa agizo hilo leo tarehe 23 Desemba 2023 alipoenda kukagua eneo kilipojengwa kituo hicho na aliambatana na Kamati ya ulizi na usalama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

“Kufuatia agizo hili, nawaagiza Wakuu wote wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji nchi nzima wafanye uhakiki wa vituo vya mafuta kwa maana ya viwanja, mabadiliko ya matumizi ya ardhi, mchakato uliotumika, ukubwa wa viwanja, ukaribu wa kituo kimoja na vituo vingine na ukaribu wa maeneo mengine ya kutolea huduma za jamii, hali ya uendeshaji wa vituo hivyo, taarifa hiyo ifike ofisini Januari 31, 2024” amesema Silaa.

Pia Waziri Silaa amewaagiza wafanyabiashara ya mafuta nchini wafanye uhakiki wa vituo vyao na Mafuta, mchakato wa namna walivyopata ardhi wanayotumia na kuwasilisha taarifa hiyo Ofisini kwake ifikapo tarehe 31 Januari 2024.

Aidha, Waziri Silaa amesema ni vema watumishi wa Ardhi na wafanyabiashara hiyo waheshimu Sheria za nchi kwa vitendo kwa kuwasikiliza watu wasio na sauti ili wapate haki zao katika masuala ya ardhi.

“Rais Samia Suluhu Hassan ni mtu wa haki, anataka watu wapate haki, ameniteua mimi kusimamia haki, hebu tusimamie Sheria, kwa mdomo tukisema tunamuunga mkono Dkt.Samia Suluhu Hasan, lakini tufanye kwa vitendo kwa kuwasililiza wale ‘the voiceless, sisi tumewekwa hapa kuwa voice of the voiceless” amesema Silaa.

Naye mkaazi wa eneo hilo la Mikocheni, Stephen Rupia amesema wananchi wa eneo hilo hawakushirikishwa kwenye hatua yeyote ambayo ilitakiwa wananchi washirikishwe.

“Tupo hapa eneo hili lilikuwa na ukuta na miti mbele na lilikuwa eneo la mtu kwa matumizi yake, hatukuona bango la kubadilisha matumizi ya eneo hili kujenga kituo hiki cha mafuta” amesema Rupia.

Akizungumza kwa niaba ya mmiliki wa kituo hicho cha Mafuta Mhandisi Stanley Kitundu amesema wameyapokea maelekezo ya Mhe. Waziri mwenye dhamana ya ardhi na watayatekeleza na kuongeza kuwa kituo chao kimekamilika kwa asilimia 100 lakini kilikuwa hakijaanza kufanyakazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!