Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao
ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the love

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri vijana nchini Tanzania kunoa ujuzi wao wa karne ya 21 ili kufanikiwa katika soko la kisasa la kiushindani la ajira. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

 Akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule za Sekondari za Feza yaliyofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki, Zaipuna alisema ujuzi wa karne ya 21 ni pamoja na kufikiri kwa kina, ubunifu, ushirikiano, mawasiliano, teknolojia ya habari, uongozi, na stadi za maisha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule za Feza Girls na Feza Boys akipokea zawadi kutoka kwa Joshua Zaipuna baada ya kutoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

 “Mkiwa na ujuzi huu, nina hakika kabisa kwamba mtafaulu katika shughuli zenu za maisha iwe mnataka kuajiriwa au kujiajiri. Mtawavutia waajiri na wawekezaji na kwa moyo wa kuendelea kujifunza, mtaimarika siku hadi siku na kujiongezea thamani,” Zaipuna alisema.

 Aliongeza, “Kwa miaka mingi, nimekuwa sehemu ya Shule za Feza na ninathamini sana msisitizo ambao shule inaweka katika elimu ya maisha na maendeleo, ushirikiano na jamii na ukuzaji wa stadi za uongozi, sifa ambazo naamini zitakuwa na athiri chanya kwa watoto wetu kwa miaka mingi ijayo,” alisema.

 Zaipuna alibainisha kuwa maisha ni safari na kuwataka vijana hao kufanya kazi kwa bidii na kuongeza kuwa wanaweza kufikia chochote wanachokusudia endapo wataendelea kuwa na nidhamu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule za Feza Girls na Feza Boys akimkabidhi cheti mwanafunzi bora katika uongozi Najat Ngairi (wa pili kushoto), wakati wa Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaama. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Shule za Feza Tanzania, Ali Nungu na kulia ni Mkuu wa Shule ya Feza Girls, Ibrahim Zanga.

 “Nilianza safari yangu takriban miongo mitano iliyopita. Miaka 32 iliyopita, nilihitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kilakala, Morogoro. Siku hii imenifanya kutafakari maisha yangu yote tangu nilipohitimu mwaka 1991,” alisema.

 Aliwataka wanafunzi hao kujiamini, kufuata nafsi zao na kamwe wasipoteze maadili na kanuni walizopandikizwa wakiwa shuleni.

 Alibainisha kuwa baadhi ya vitu ambavyo vimesaidia kupanda daraja la mafanikio ni pamoja na nidhamu, bidii, uadilifu, ubora katika kila kazi iwe kubwa au ndogo na kuendelea kujifunza mambo mbalimbali.

 “Licha ya vikwazo ambavyo mmekumbana navyo mkiwa hapa, mmeibuka kuwa nyota zinazongaa. Katika miaka yenu yote katika Shule za Feza, mmeonyesha dhamira isiyoyumba kwa kuendela kufanya vyema. Mafanikio haya ni uthibitisho wa bidii zenu” alisema.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule za Feza Girls na Feza Boys akimpongeza mwanafunzi aliyesoma risala Iqra Jamal wakati wa Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaama. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Shule za Feza Tanzania, Ali Nungu na kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Feza Girls, Ibrahim Zanga.

 Aliwashauri wahitimu hao kuchangamkia fursa zinazowajia huku akiongeza kuwa mafanikio hayapimwi kwa alama au sifa tu, bali pia kwa matokeo yanayopatikana katika maisha ya wengine.

 Awali, Naibu Mkurugenzi wa Shule za Feza, Ali Nungu aliwataka wahitimu kuendeleza miiko ya shule hiyo ilikuleta mabadiliko katika njia watakayochagua.

 Aliwapongeza walimu wa shule hiyo, wafanyakazi wengine na wazazi ambao walichukua jukumu kubwa katika safari ya wahatimu hao na kuwataka wahitimu kuamini katika uwezo wao.

Alionyesha imani kwamba kwa tabia zao nzuri, uwezo bora wa kitaaluma na ustahimilivu, watakuwa wakakamavu na wenye shauku katika kutimiza ndoto zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!