Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC CCM yateua wagombea uenyekiti mikoa, wilaya
Habari za Siasa

NEC CCM yateua wagombea uenyekiti mikoa, wilaya

Spread the love

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa leo Jumatano kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama kwa ngazi ya mkoa na wilaya.

Nafasi zinalenga kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amesema nafasi ya mwenyekiti wa mkoa wa Arusha: wanachama waliojitokeza 89.

Walioteuliwa ni: Dk. Daniel Mirisho Pallangyo, Loy Thomas Sabaya, Solomon Olesendeka Kivuyo na Edna Israel Kivuyo.

Mkoa wa Mbeya: Wanachama waliojitokeza 48, Walioteuliwa ni:  Felix Jackson lyaniva,  Patrick Adkin Mwalunenge na Fatuma Ismail Kasenga.

Mkoa wa Mwanza: Wanachama waliojitokeza 109, Walioteuliwa ni: Michael Lushinge Masanja (Smart),  Sabana Lushu Salinja, Dkt. Anjelina William Samike, Elizabeth Watson Nyingi na David Mayala Mulongo.

Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya

Wilaya ya Mpanda: Wanachama waliojitokeza 36, Walioteuliwa ni:  Hamis Chande Soud, Joseph Aniseth Lwamba, Josephina Yusuph Baraga na Emmanueli David Manamba.

Wilaya ya Kusini Unguja: Wanachama waliojitokeza 15, Walioteuliwa ni: Maryam Suleiman Haji, Ali Timamu Haji na Mohammed Haji Hassan.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimepongeza Serikali inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

error: Content is protected !!