Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 33 wanusurika ajali ya ndege Mikumi
Habari MchanganyikoTangulizi

33 wanusurika ajali ya ndege Mikumi

Spread the love

JUMLA ya abiria 30, marubani wawili na mhudumu mmoja wamenusurika kifo katika ajali ya ndege iliyotokea leo saa 3:40 asubuhi katika Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ndege hiyo ya kampuni ya Unity Air 5H-MJH aina ya EMBRAER 120 iliyokuwa ikitokea Zanzibar ilipata tatizo la kiufundi wakati ikitua katika kiwanja cha ndege cha Kikoboga kilichopo katika hifadhi hiyo ya Mikumi.

Taarifa iliyotolewa Afisa Uhifadhi Mwandamizi Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Catherine Mbena imesema juhudi kubwa zimefanywa na marubani wa ndege hiyo pamoja na maofisa katika kiwanja hicho kuhakikisha kuwa hakuna madhara yatakayotokea kutokana na ajali hiyo.

“Abiria wote 30, marubani wawili, pamoja na mhudumu wa ndege hiyo wako salama na wanaendelea na ratiba yao ya kufanya utalii hifadhini.

“Matumizi ya kiwanja pamoja na shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida,” amesema na kuongeza kuwa;.

“TANAPA imefanya taratibu zote za kuwasiliana na idara ya uchunguzi wa ajali za ndege itiyopo Wizara ya Uchukuzi –(AAIB) kwa ajili ya taratibu zingine na uchunguzi zaidi juu ya tukio hili,” amesema.

Amesema shirika linatoa shukrani kwa kikosi cha zimamoto na uokoaji Mikumi kwa ufanisi mkubwa katika changamoto hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye vvu, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

error: Content is protected !!