Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Latra yatangaza kupanda kwa nauli za daladala, mabasi
Habari MchanganyikoTangulizi

Latra yatangaza kupanda kwa nauli za daladala, mabasi

Spread the love

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli mpya ya mabasi ya mijini na masafa marefu ambapo safari ambazo hazizidi kilomita 10 gharama yake itakuwa Sh 600 badala ya Sh 500. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Safari zinazozidi kilomita 10, yaani kilomita 11 hadi kilimota 15 sasa itakuwa Sh 700 badala ya Sh 550, kilomita 16 hadi kilomita 20 nauli itakuwa Sh 800 badala ya Sh 600, kilomita 21 hadi kilomita 25 ambayo nauli yake ni Sh 700, nauli itakuwa Sh 900 na kilomita 26 hadi kilomita 30 nauli itakuwa TZS 1,100 kutoka Sh 850, kilomita 31 hadi kilomita 35 nauli itakuwa Sh 1,300 badala ya Sh 1,000 na kilomita 36 hadi kilomita 40 nauli itakuwa Sh 1,400 badala ya Sh 1,100.

Ametangaza mabadiliko hayo Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jumatatu mkoani Arusha ikiwa ni mrejesho wa kikao kilichofanyika kati ya LATRA na wadau wa usafirishaji.

LATRA imesema kwa upande wa nauli za wanafunzi, gharama imebaki kuwa shilingi 200 kama hapo awali.

Aidha, LATRA imewaelekeza madereva kufuata taratibu na masharti yaliyotolewa ikiwemo kutotoza nauli iliyopendekezwa pamoja na kuzingatia usafi kwa kupulizia dawa ili kuua wadudu kwenye magari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

error: Content is protected !!