Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda: Chama kitafuata mkondo wake kuhusu Gekul
Habari za SiasaTangulizi

Makonda: Chama kitafuata mkondo wake kuhusu Gekul

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema taratibu zitafuata mkondo wake kupitia mamlaka za nidhamu kuhusu tuhuma za udhalilishaji zinazomkabili Mbunge wa Babati mjini, Pauline Gekul (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 27 Novemba 2023 jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda amesema chama hicho kina kanuni na taratibu.

“Kuhusu mbunge wa babati mjini, chama chetu kina kanuni na taratibu… na sisi ngazi ya Taifa tunajua kuna mamlaka kuanzia ngazi ya tawi alilotokea, kuanzia wilaya hadi kwenda mkoa na itakapofikia Taifa tutatoa taarifa ya nini kimetokea lakini kanuni zipo na tuna timu ya mamlaka ya nidhamu na kama jambo litabainika basi taratibu zitafuata mkondon wake,” amesema Makonda.

Kauli hiyo ya CCM imekuja wakati mbunge huyo akidaiwa kutoa maelekezo kwa kundi la vijana kumdhalilisha kwa kumpiga na kumwingiza chupa sehemu ya haja kubwa na kumtishia kumpiga mfanyakazi wake risasi, Hashim Ally.

Tuhuma dhidi ya Gekul ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, zilianza kusambaa mitandaoni hivi karibuni na video yenye urefu wa takribani dakika 4: 03 zilimuonyesha kijana Ally akielezea unyama aliofanyiwa huku akiomba msaada.

Wakati tuhuma hizo zikizidi kushika kasi huku watetezi wa haki za binadamu wakijitokeza kulisemea sakata hilo, Rais Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wa naibu waziri huyo.

Aidha, Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Kamishna msaidizi George Katabazi naye amenukuliwa akiwataka wakazi wa mjini Babati kuwa watulivu wakati wao wakiendelea na uchunguzi wa tukio la kijana huyo.

“Tunawaomba watu watupe nafasi tufanye kazi yetu, hakuna mtu yetote aliye juu ya sheria hapa nchini, wasijali tunasimamia upatikanaji wa haki kwa mujibu wa sheria zilizopo,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

error: Content is protected !!