Saturday , 18 May 2024
Home Kitengo Biashara Dk. Biteko aipongeza NMB kwa ubunifu, uwekezaji katika teknolojia
BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa ubunifu, uwekezaji katika teknolojia

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameipongeza benki ya NMB kwa kuwa wabunifu kwenye utoaji huduma pamoja na kuwekeza kwenye teknolojia. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Dk. Biteko ametoa pongezi hizo leo tarehe 24 Novemba, 2023 alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dk. Biteko ameiasa NMB kuangalia uwezekano wa kusaidia uwekezaji wa miradi mbalimbali ya umeme hususani ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji wa umeme, ili kuwezesha upatikanaji umeme wa uhakika.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amesema kuwa, lengo la ziara hiyo ni kumpongeza Dk. Biteko kwa kuteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Amesema kuwa, kwa sasa uchumi wa nchi umeimarika na unakua kwa asilimia 5.3 ambapo Tanzania ni moja ya nchi bora kwenye uwekezaji kwa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

NMB ni moja Kati ya benki zinazofanya vizuri kwenye soko la benki ambapo ina jumla ya matawi 230 na wakala elfu 24 nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet watoa msaada wa chakula Chamazi

Spread the love  JUMAMOSI ya leo Meridianbet wametua pale Chamazi Magengeni kwaajili...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB ‘yafunga ndoa’ na wanawake wanaomiliki shule, vyuo Tanzania

Spread the loveBENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!