Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Biashara Majaliwa aipongeza STAMICO kuendelea kunadi matumizi nishati mbadala
Biashara

Majaliwa aipongeza STAMICO kuendelea kunadi matumizi nishati mbadala

Spread the love

Waziri  Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  amelipongeza Shirika la Madini la Taifa STAMICO  kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati  Mbadala  kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema STAMICO  imetumia fursa nzuri kwa kuungana na Wahiriri katika Mkutano wao wa Mwaka kuhamasisha  matumizi ya Nishati  ya Rafiki Briquette  ili kuokoa mazingira.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba 2023 kwenye Mkutano Mkuu wa Saba wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika kwa siku tatu Mkoani Lindi.

Amesema kuwa STAMICO imejipambanua katika kuhakikisha inaleta nishati mbadala , kwa kuwa nishati hiyo itaokoa miti mingi inayotumika kutengeneza mkaa.

“Mmetumia Jukwaa sahihi kufanya hamasa ya mkaa huu, niwapongeze sana kwa jinsi mlivyojitahidi kuleta mkaa utokanao na mabaki ya mkaa utakaozuia ukataji wa miti  mingi kwa kuzalisha mkaa kidogo” Amesisitiza  Waziri Mkuu.

Akiongea kwa niaba ya STAMICO  Afisa Masoko  wa STAMICO, Mark Stephano amesema Shirika limejipanga  vyema  kuhakikisha nishati hiyo inasambaa katika maeneo mengi nchini Tanzania ikiwemo mkoa wa Lindi.

“Tayari  Shirika limeleta na kuifunga  Mitambo  mikubwa miwili  ya kuzalisha  Mkaa wa Rafiki Briquettes yenye uwezo wa kuzalisha mkaa tani 20 kwa saa, ambayo imefungwa katika mkoa wa Pwani na Songwe  eneo la Kiwira” amesema Stephano.


Jukwaa la Wahariri Tanzania limekutana Mkoani lindi katika Mkutano wake Mkuu wa saba tangu kuanzishwa kwake wenye kaulimbiu isemayo ‘Uandishi wa Habari, Gesi na Uchumi Endelevu kwa Nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Sloti ya Wild 81 malipo kwa njia 81 Meridianbet kasino

Spread the love Meridianbet kuna mchezo wa sloti wa kusisimua sanaambao utakufurahisha....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Biashara

Meridianbet watoa msaada wa chakula Chamazi

Spread the love  JUMAMOSI ya leo Meridianbet wametua pale Chamazi Magengeni kwaajili...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB ‘yafunga ndoa’ na wanawake wanaomiliki shule, vyuo Tanzania

Spread the loveBENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha...

error: Content is protected !!