Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Biashara NMB yawanoa wahariri kuhusu bima ya afya, mazishi
Biashara

NMB yawanoa wahariri kuhusu bima ya afya, mazishi

Spread the love

BENKI ya NMB imewanoa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu matumizi ya huduma mpya za bima ya afya pamoja na bima ya mazishi ambazo zimetajwa kuwa mkombozi kwa Watanzania wenye kipato kidogo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamejiri leo tarehe 13  Novemba 2023 lkatika Mkutano Mkuu wa Saba wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika mkoani Lindi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack wakimsikiliza Meneja wa NMB Kanda ya Kusini – Faraja Ng’ingo alipotembelea banda la benki hiyo katika uwanja wa Ilulu mjini Lindi ambako kunafanyika Mkutano mkuu wa Saba wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Akiwasilisha mada kuhusu benki hiyo ambayo ni moja ya wadhamini wa mkutano huo, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Faraja Ng’ingo amesema huduma hizo zinalenga kuboresha afya za Watanzania.

Akifafanua kuhusu huduma ya Bima ya Afya ambayo inatolewa na benki hiyo kupitia kampuni ya Strategis, Ng’ingo amesema wateja wa benki hiyo wanaweza kujiunga na huduma za bima ya afya kwa gharama ya Sh 200,000 pekee kwa mwaka.

“Hii sio bima ya mkoani tu. Unatibiwa hospitali zote za ngazi ya rufaa ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili,” amesema.


Ameongza kuwa kwa gharama hiyo ya Sh 200,000 inawezesha familia ya baba, mama na watoto wa nne kupata huduma hizo za afya.

Amesema iwapo kutakuwa na ongezeko la watoto, kila mmoja atatakiwa kulipiwa nyongeza ya Sh 80,000.

Ameongeza kuwa katika magonjwa sugu ya muda mrefu, bima hiyo itawezesha mgonjwa kutibiwa kwa muda wa mwaka mmoja.

Aidha, akifafanua kuhusu huduma za bima ya mazishi, Afisa Uhusiano wa NMB wa Benki hiyo Mkoa wa Lindi, Christina Silayo amesema wanufaika wa huduma hiyo wanaweza kupewa mkono wa pole kuanzia milioni moja hadi milioni tano.

Afisa Uhusiano wa NMB wa Benki hiyo Mkoa wa Lindi, Christina Silayo akizungumza katika mkutano huo.

Amesema huduma hiyo inapatikana kutokana na wanufaika kujiunga kwenye kikundi na kujipangia kiwango cha mchango kuanzia Sh 2000 hadi Sh 8,500.

Amesema mnufaika wa huduma hiyo ambaye pia anaweza kuwa msimamizi wa mirathi,  atapata mkono wa pole kwa kuwa na uthibitisho wa cheti cha kifo cha mteja aliyejiunga na huduma hiyo enzi za uhai wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

Biashara

Haya ni Maajabu ya sloti ya Jade Valley ya kasino ya mtandaoni Meridianbet

Spread the love  JADE Valley ni mchezo wa sloti wenye nguzo tano...

Biashara

Washindi wa Serengeti Maokoto ndani ya Kizibo Dar, Dodoma walamba mzigo

Spread the love Mustapha Ally, Mkazi wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma...

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

error: Content is protected !!