Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Balile: Wanafunzi wapewe motisha kujiunga na tasnia ya habari
Habari Mchanganyiko

Balile: Wanafunzi wapewe motisha kujiunga na tasnia ya habari

Spread the love

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) Deodatus Balile amesema kuwa ni muda muafaka wa kuwapa motisha wanafunzi katika tasnia ya habari. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Balile ameyasema hayo leo Ijumaa katika Chuo kikuu cha Tumaini (Tudarco) baada ya kumkabidhi zawadi Mwanafunzi Patson Andungalile  aliyefanya vizuri katika masomo ya uandishi wa habari chuoni hapo.

“Tumeshuhudia tasnia nyingine wafanyakazi, wanafunzi wanaofanya vizuri hupewa zawadi sasa ni wakati muafaka wa kuwatia moyo wanafunzi katika tasnia hii ili naye akimaliza ajue kuwa anatambulika” amesema Balile.

Balile amewataka wanafunzi wa taalama ya habari kuhakikisha wanajiandaa vizuri ili wakiingia kwenye vyombo vya habari wapate nafasi ya kuajiriwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!