Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Muswada sheria ya tume uchaguzi, msajili wa vyama yatinga bungeni
Habari za Siasa

Muswada sheria ya tume uchaguzi, msajili wa vyama yatinga bungeni

Spika Dk. Tulia Ackson
Spread the love

MUSWADA wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, imesomwa kwa mara ya kwanza, bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Miswada hiyo ni miongoni mwa miswada mitano ya sheria mbalimbali, iliyosomwa kwa mara ya kwanza, bungeni jijini Dodoma, leo tarehe 10 Novemba 2023.

Ikisoma miswada hiyo kwa mara ya kwanza, Ofisi ya Katibu wa Bunge, imesema Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, umewasilishwa kwa lengo la kubainisha muundo, majukumu, utaratibu wa upatikanaji wajumbe wa tume , sifa za mkiurugenzi wa uchaguzi na mambo mengine yanayohusiana na tume hiyo.

Kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa, imesema umewasilishw akwa lengo la kuimarisha nafasi ya msajili wa vyama vya siasa, kama msimamizi wa mienendo ya vyama pamoja na kuimarisha uzingatiaji wa sheria na kanuni katika vyama hivyo.

Miswada mingine iliyosomwa kwa mara ya kwanza, ni wa sheria ya uwekezaji wa umma. Muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali zipatazo nne kwa lengo la kuondoa mapungufu ambayo yamejitokeza wakati wa utekelezaji wa baadhi ya masharti katika sheria hizo.

Baada ya miswada hiyo kutumwa, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alisema itapelekwa katika kamati husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

“Miswada mitano imesomwa kwa mara ya kwanza, kama ilivyoada miswada hii itapelekwa kwenye kamati zinazohusika. Nitaelekezea katika kamati husika muda utakapofika,” amesema Spika Tulia.

Miswada hiyo imewasilishwa bungeni baada ya wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi nchini, kuishauri serikali izifanyie marekebisho sheria hizo ili kuondoa mapungufu yake kabla ya chaguzi zijazo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!