Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watakaoharibu alama za barabarani, miundombinu kukiona cha moto
Habari Mchanganyiko

Watakaoharibu alama za barabarani, miundombinu kukiona cha moto

Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka wakuu wa wilaya nchini kutoka elimu kwa wananchi ngazi ya vijiji,kataka na, Tarafa ikiwemo jamii ya wafugaji kulinda alama za barabarani na miundombinu iliyopo ili kuhepuka uharibifu na ajali zisizokuwa za lazima. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo leo tare he 6 Oktoba,2023 wakati akikagua barabara yenye urefu wa mita 400 iliyojengwa makao makuu ya wilaya ya Songwe (Mkwajuni) iliyojengwa na wakala wa barabara nchini (TANROADS)  mkoani Songwe kwa gharama ya Tsh, Milioni 320.

Amesema  wakuu wa wilaya watasaidia kuhepusha  ajali endapo watatoa elimu kuanzia ngazi za vitongoji hadi Tarafa wakiwemo wafugaji wenye tabia ya kupitisha kifugo barabarani na kuharibu miundombinu.

Amesema miundombinu ya barabara ni muhimu kwa madereva kwani zinaonesha maeneo hatarishi na hata wapita kwa miguu wanakuwa na uhakika wa usalama wao pindi wanapovuka upande wa pili kwa kuangalia alama zilizopo.

Akizungumzia suala hilo, mkuu wa wilaya ya Songwe Solomon Itunda,amesema ameyapokea maagizo hayo huku akisisitiza kuwa waharibifu wa miundombinu ni sawa na wahujumu uchumi hivyo atahakikisha anatoa elimu kwa jamii na kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kuharibu miundombinu.

Aidha Itunda amemshukuru Rais Dr, Samia Suruhu kwa kuleta suruhu kwenye wilaya ya Songwe kwa kuwapatia fedha Bilion 1.3 zinazotumika kujenga miundombinu ya barabara na madaraja fedha zilizotendewa haki na Tanroads, kazi iliyopo ni kuhakikisha miundombinu haiharibiwi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!