Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia
Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza za kukutwa wakitengeneza noti bandia za nchini Zambia. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 3 Oktoba 2023, Kamanda wa polisi mkoani Songwe, Teopista Malya amesema watuhumiwa hao wamekamatwa leo mchana katika mtaa wa Nazareth kata ya Mwakakati halmashauri ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani hapa.

Bila kuwataja majina watuhumiwa, Kamanda Malya amesema mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 48, ni mkazi wa Mpulungu Zambia  na wa pili (49) mkazi wa Msongwa Tunduma. Wote wamekutwa na noti 12  za Kwacha zenye thamani ya Kwacha 50 za nchini Zambia.

Aidha, Kamanda Malya amesema watuhumiwa hao pia walikamatwa na karatasi 10 za ukubwa wa A4 zilizochapishwa kwacha 50  kwa idadi ya noti bandia 36 kwenye karatasi hiyo ambayo pia ilichapishwa noti 4 zenye thamani ya kwacha 100 zenye namba EJ228951989 na EJ220684457 na EJ17714847.

RPC Mallya

Amesema pia waliwakamata wakiwa na visu viwili, mkasi wa kukatia karatasi, vitambulisho viwili vya Taifa la Zambia, vyenye namba Z.7714847 na Z,1600353.

Hata hivyo, amesema jeshi hilo linaendelea kufuatilia mtandao mzima wa kundi hilo la kutengeneza noti bandia na kwamba waliokamatwa watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!