Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani, wenyeviti wa vijiji watengewa posho bilioni 22.5
Habari za Siasa

Madiwani, wenyeviti wa vijiji watengewa posho bilioni 22.5

Dk. Festo Dugange
Spread the love

SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2023/ 2024 imetenga kiasi cha Sh 22.5 bilioni kwa ajili ya kulipa posho za madiwani na wenyeviti wa vijiji katika halmashauri 168. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo…(endelea).

Hayo yameelezwa leo Ijumaa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dk. Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM).
Waitara alihoji, ni lini serikali itaongeza posho za madiwani na wenyeviti wa vijiji.

Akijibun swali hilo, Naibu Waziri huyo amesema serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na madiwani na wenyeviti wa vijijini katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

“Hivyo, kwa mujibu wa sheria ya mamlaka za serikali za mitaa sura ya 290, kila halmashauri inatakiwa kuweka utaratibu wa kuwalipa posho, madiwani na wenyeviti wa mtaa na vijiji kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri.

Dugange ameongeza kuwa kutokana na changamoto za mapato kwenye halmashauri nyingi nchini, serikali ilianza kutenga bajeti katika mwaka wa fedha 2021 hadi 2022 kwa ajili ya kulipa posho za madiwani pamoja na wenyeviti wa vijiji.

“Serikali inaendelea kuzijengea uwezo mamlaka za serikali za mitaa ili ziweze kubuni na kuimarisha vyanzo vya mapato pamoja na kuthibiti mianya ya upotevu wa fedha kwa kutumia mifumo ya kieletroniki ya kukusanya na kutumia fedha katika kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na matumizi mengineyo ili kuongeza uwezo wa malipo kwa viongozi,” amesema.

Katika maswali ya nyongeza, Waitara alihoji kwa mwaka wa fedha ujao 2024 hadi 2025 serikali ipo tayari kuongeza posho ya madiwani na wenyeviti wa vijiji na mitaa ili kupunguza kelele za viongozi hao?.
Akijibu maswali hayo, Dugange amesema posho hizo zilipandishwa zilipandishwa lakini atakwenda kuona ni lini zilianza.

“Lakini nafahamu kwamba zilipandishwa kutoka zilipokuwa kidogo lakini sasa angalu ziko na hali nzuri yaani tunatambua kwamba zinahitajika kuongezeka zaidi ili ziweze kukidhi mahitaji na safari ni hatua, serikali linaendelea kulitatua, kutazama na kuona uwezekano huo wa kupandisha zaidi posho za madiwani.

“Kuhusu mwaka ujao wa fedha kama tutaongeza posho hizo au vinginevyo, tumelichukua… serikali tutafanya tathmini nakuona uwezekano huo na itatoa taarifa rasmi kama linawezekana ama tunahitaji kujiongezea uwezo wa posho hizo,” ameongezea Dugange.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!