Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wabunge waibana Serikali kero ya popo Dar
Habari Mchanganyiko

Wabunge waibana Serikali kero ya popo Dar

Spread the love

WABUNGE wameitaka serikali kuondoa popo waliopo maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam ili kulinda afya za wakazi wa maeneo hayo. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo…(endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo na malalamiko kwa wakazi wa maeneo ya Upanga, Sea View, Leaders Club, Kinondoni, Oysterbay, Masaki, Msasani Peninsula na maeneo mengine ya Ukanda wa Pwani kwamba popo hap wamekuwa kero kwa wananchi.

Popo hao wamedaiwa pia kusababisha uharibifu kwa kuvunja vioo vya madirisha kwenye makazi yao.

Hayo yamejiri leo Jumatatu bungeni jijini Dodoma wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Neema Mgaya aliyehoji  ni lini serikali itaondoa popo waliopo maeneo ya Upanga ili kulinda afya za wakazi wa maeneo hayo.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo, amesema Wizara imeendelea kuthibiti popo katika jiji la Dar-es-salaam kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji kuangalia ukubwa wa tatizo.

Amesema kuna aina mbili ya popo wanaosumbua ikiwamo popo wanaotumia mapango au magofu ya nyumba kama makazi yao.

Amesema katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, majaribio ya dawa tano za kunyunyizia ili kufukuza popo katika makazi yao zilitumika kati ya dawa hizo, dawa mbili(Napthalene na Bat CRP) zimeonekana kuwa na uwezo wa kuwafukuza popo hao na juhudi zaidi zinaendelea kwa kushirikiana na wadau kwenye maeneo husika.

“Utafiti huu umekamilika sasa jukumu lililopo mbele yetu ni wakuhakikisha kwamba wadau wote husika na kukubaliana na jambo hili, lipo kwenye halmashauri zetu zinachukua hatua za kuhakikisha kwamba tunasambaza dawa hizi kwa wananchi ili tuweze kukabiliana na tatizo hili. Niombe wadau wote husika tushirikiane ili tuweze kuondokana na tatizo hili,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!