Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ummy Mwalimu aunda kamati kuchunguza malalamiko ya madaktari waliofelishwa
Afya

Ummy Mwalimu aunda kamati kuchunguza malalamiko ya madaktari waliofelishwa

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo Jumatatu ametangaza ameunda Kamati huru yenye wajumbe 13 ili kuchunguza malalamiko ya madaktari watarajali (Intern Doctors) kuhusu kufeli mitihani ya kabla na baada ya mafunzo ya Internship ili waweze kupata usajili wa kudumu wa Baraza la Madaktari Tanganyika-MCT.

Kamati hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja na kufuata hadidu za rejea zilizoainishwa na Wizara ili kuchunguza msingi wa malalamiko yaliyotolewa na Madaktari tarajali katika barua yao waliyoielekeza kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Maryam Mudhihir …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa yake Waziri wa Afya,  iliyotumwa kwenye vyombo vya habari leo tarehe 14 Agosti 2023 amesema kuwa kamati hiyo huru itaongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Mstaafu, Profesa Mohamed Bakari.

“Kamati hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja na kufuata hadidu za rejea zilizoainishwa na Wizara ili kuchunguza msingi wa malalamiko yaliyotolewa na Madaktari tarajali katika barua yao waliyoielekeza kwa Rais Samia Suluhu” imeeleza taarifa hiyo.

MCT inatekeleza wajibu wa  sheria ya madaktari,madaktari wa meno na wataalamu wa Afya shirikishi ,sura 152 ya mwaka 217, pamoja na kanuni zake za mitihani na usajili za mwaka 2018.

Sheria mpya inahitaji mtihani wa usajili wa muda ili kuhakikisha kuwa madaktari wanaopata umahiri husika kutoka Desemba 2020 hadi Desemba 2022 ambapo asilimia 68 hadi 99 ya madaktari wanaofanya mitihani hiyo wamefaulu.

Hata hivyo, katika mtihani wa Machi 2023, ni asilimia 42 tu ya watahiniwa 640 waliofaulu.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa “Kamati itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto zilizobainika.

Wajumbe wa kamati ni wanataaluma wenye uzoefu katika sekta ya afya kutoka vyuo vikuu na hospitali”

Waziri Ummy amesema kuwa wakati kamati inatekeleza majukumu yake, mafunzo ya utarajali yataendelea kama ilivyoelezewa na sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Kambi ya matibabu ya kibingwa Ruangwa yaacha vilio, DC atoa ombi JAI

Spread the loveMKUU wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma amefunga rasmi kambi...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Afya

Mbunge ataka huduma Ultrasound itolewe bure kwa wajawazito

Spread the loveMBUNGE wa Viti Maalum, Esther Malleko, ameitaka Serikali kutoa bure...

Afya

Vituo 13 vyasitishiwa mkataba madai kutaka kupiga bilioni 4 za NHIF

Spread the loveVITUO vya kutoa huduma za afya 13, vimesitishiwa mikataba ya...

error: Content is protected !!