Monday , 20 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awapangia vituo vya kazi mabalozi 10, Dk. Nchimbi arejeshwa nyumbani
Habari za Siasa

Rais Samia awapangia vituo vya kazi mabalozi 10, Dk. Nchimbi arejeshwa nyumbani

Dk. Emmanuel Nchimbi
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi mabalozi wakiwemo mabalozi wateule sita aliowateua tarehe 10 Mei 2023 na kuwabadilisha vituo vya kazi mabalozi wanne. Anaripoti Maryam Mudhihiri…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 11 Agosti 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imebainisha kuwa mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi ni; Balozi Fatma Mohammed Rajab kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman. Balozi Rajab anachukua nafasi ya Balozi Abdallah Abasi Kilima ambaye amestaafu.

Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada. Balozi Sokoine anachukua nafasi ya Balozi Dk. Mpoki Ulisubisya ambaye amestaafu.

Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.

Wengine walioteuliwa ni Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Rwanda. Meja Jenerali Mwaisaka anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo ambaye amehamishiwa Cairo, Misri.

Gelasius Gaspar Byakanwa (balozi mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Burundi. Byakanwa anachukua nafasi ya Balozi Jilly Maleko ambaye amestaafu.

Habibu Awesi Mohamed (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar. Mohamed anachukua nafasi ya Balozi Mahadhi Juma Maalim ambaye amehamishiwa Kuala Lumpur, Malaysia.

Imani Salum Njalikai (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria. Njalikai anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu ambaye amestaafu.

Hassan Iddi Mwamweta (Balozi Mteule) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani. Mwamweta anachukua nafasi ya Balozi Abdallah Saleh Possi ambaye amehamishiwa Geneva, Uswisi.

Dk. Mohamed Juma Abdallah (Balozi Mteule) kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Abdallah anachukua nafasi ya Balozi Ali Jabir Mwadini ambaye amehamishiwa Paris, Ufaransa.

Aidha, mabalozi waliohamishwa vituo ni pamoja na; Balozi Ali Jabir Mwadini kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa. Balozi Mwadini anachukua nafasi ya Balozi Dk. William Shelukindo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri. Balozi Meja Jenerali Makanzo anachukua nafasi ya Balozi John Emmanuel Nchimbi ambaye anarejea nyumbani.

Balozi Abdallalh Saleh Possi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi. Balozi Possi anachukua nafasi ya Balozi Maimuna Tarishi ambaye amemaliza mkataba wake.

Balozi Dk. John Stephen Simbachawene kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda. Balozi Simbachawene anachukua nafasi ya Balozi Dk. Aziz P. Mlima ambaye amestaafu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabalozi hao wateule wataapishwa tarehe 16 Agosti, 2023 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Chamwino – Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

error: Content is protected !!