Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Singida atahadharisha wafanyabiashara kukopa katika taasisi zilizosajiliwa
Habari Mchanganyiko

RC Singida atahadharisha wafanyabiashara kukopa katika taasisi zilizosajiliwa

Spread the love

WAFANYABIASHARA wanaotarajia kukopa ili kuendesha biashara wameshauriwa kuchukua mikopo kwenye taasisi za kifedha ambazo zimesajiliwa na Benki Kuu (BoT). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi yanayofanyika kikanda katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema taasisi zote zinazotoa mikopo zinatakiwa kuwa zimesajiliwa na Benki kuu ya Tanzania na lazima leseni za taasisi hizo ziwe sehemu ya wazi kwa nia ya mteja kujiridhisha na usajili wa taasisi husika.

Mkuu huyo wa mkoa amesema taasisi ambazo zinatoa fedha bila kuwa na usajili wa BoT zinavunja sheria ya nchi na kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwatapeli wale ambao wamekuwa wakikopa pesa hizo kwani hawastahili kutoa mikopo hiyo.

Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya Msingi Nzuguni, ambaye hakutaja jina lake litajwe amesema kuwa walimu wamekuwa wahanga zaidi katika mikopo umiza na wakati mwingine hulazimika kuwapatia wale wanaowakopesha kadi za benki na kila mshahara unapoingia hulazimika kukatwa pesa hizo.

Aidha, amesema kutokana na kupata elimu ya kutosha juu ya ukopaji sasa watakuwa makini katika kutambua taasisi sahihi ambazo zipo kisheria katika kukopesha badala ya kujitumbukiza katika mikopo umiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali kuwafagilia njia wawekezaji sekta ya mawasiliano

Spread the love  SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili...

Habari Mchanganyiko

Elimu ya utunzaji wa mazingira ipewe kipaumbele kwa watoto

Spread the love  JAMII imetakiwa kuwajengea Watoto tabia ya utunzaji wa mazingira...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

error: Content is protected !!