Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ataka vijana watumike kuleta mageuzi uchumi Afrika
Habari za Siasa

Rais Samia ataka vijana watumike kuleta mageuzi uchumi Afrika

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, amezitaka nchi za Afrika kutumia vijana katika kuleta mageuzi ya kiuchumi barani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi, ametoa wito huo leo tarehe 26 Julai 2023 wakati akihutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu rasilimali watu, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Idadi kubwa ya vijana tulionayo Afrika ni fursa ya kipekee kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi, badala ya kuwaacha vijana hawa wavuke hizo bahari wapigwe njiani , wazamishwe kwamba wanaenda Ulaya kutafuta maisha bora, maisha bora watayapata Afrika tukiwaendeleza,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amezitaka nchi za Afrika kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza rasilimali watu kwa manufaa ya bara hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!