Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Mkuu aipongeza NBC kwa kusaidia afya ya uzazi
Habari Mchanganyiko

Waziri Mkuu aipongeza NBC kwa kusaidia afya ya uzazi

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuandaa mbio za NBC Marathon ambazo zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia afya ya uzazi na saratani ya shingo ya kizazi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza muda mfupi baada ya mbio hizo kumalizika jijijini Dodoma leo Jumapili, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kuiunga mkono kwenye kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili jamii.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimvisha medali mmoja wa washindi wa NBC Dodoma Marathon 2033. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pindi Chana (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi. Mbio za mwaka huu zimefanikiwa kukusanya shilingi milioni 500 zitakazotumika kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na afya ya uzazi kwa wanawake.

“Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na benki ya NBC. Tunafurahishwa na ushirikiano mzuri kati ya Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, Taasisi ya Benjamini Mkapa pamoja na chama cha riadha Tanzania ambao umekuwa ukiwezesha kukusanya fedha kwa ajili ya kusaida mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na mwaka huu likiongezeka eneo la afya ya uzazi. Serikali inapongeza jitihada hizi nzuri,” amesema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akishiriki katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2023 pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi (wa pili kulia). Wengine wa kwanza kulia ni mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na kushoto ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri. Mbio za mwaka huu zimefanikiwa kukusanya shilingi milioni 500 zitakazotumika kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na afya ya uzazi kwa wanawake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Theobald Sabi amesema baada ya kumalizika kwa mbio z mwaka huu,  benki hiyo inayo furaha kuandaa mbio za mwaka ujao ikiwa ni baada ya kuandaa mbio hizo kwa mara tatu mfululizo kwa ufanisi.

“Baada ya kuandaa mbio hizi kwa mara ya nne mfululizo, tunayo furaha kuanza maandalizi ya msimu wa nne. Fedha zilizopatikana leo shilingi milioni 500 zitatumika kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi,” amesema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadhami ni wa NBC Dodoma Marathon 2023 pamoja na viongozi wa Benki ya NBC na viongozi wa mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya kumalizika kwa mbio hizo. Mbio za mwaka huu zimefanikiwa kukusanya shilingi milioni 500 zitakazotumika kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi na afya ya uzazi kwa wanawake.

Ameongeza “Tunaendelea na jitiahada za kuunga mkono mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi. Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi  milioni 500 zilizosaidia kufikia  upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake zaidi ya 23,500 na matibabu kwa zaidi ya wanawake 1,300.

“Benki ya NBC inawapongeza na kuwashuru washiriki wote kutoka nje na ndani ya nchi kwa kuweza kufanikisha mbio za mwaka huu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!