Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwanafunzi mbaroni akidaiwa kumuua mwalimu aliyemtaka akaswali
Habari MchanganyikoTangulizi

Mwanafunzi mbaroni akidaiwa kumuua mwalimu aliyemtaka akaswali

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kinamshikilia mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Qiblaten Kawe, Mohamed Jabir, kwa tuhuma za kumuua Mwalimu wake, Hassan Mohamed. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Ijumaa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema tukio Hilo limetokea alfajiri ya tarehe 20 Julai 2023.

Ni naada ya Jabiri kudaiwa kumchoma kwa kisu Mwalimu wake maeneo ya shingoni kitendo kilichopelekea kupoteza maisha.

“Mtuhumiwa alitekeleza kauaji hayo saa 11.10 alfajiri baada ya kumshambuliwa Mwalimu (Patron), aliyekuwa akiwahimiza wanafunzi  wakati wa kuhudhuria ibada ya alfajiri. Majeruhi alifariki wakati anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na mwili wake umehifadhiwa hospitalini hapo,” amesema Kamanda Muliro.

Kamanda Muliro amesema mtuhumiwa atafaikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!