Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu aitwa na DCI
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu aitwa na DCI

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amedai kuitwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam kesho tarehe 20 Julai 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa jana tarehe 18 Julai 2023 kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilimtaka Mwanasheria huyo machachari kufika katika ofisi hiyo kutokana na kauli alizozitoa tarehe 15 Julai 2023 na kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tarehe 15 Julai 2023, Lissu anadaiwa kutumia maneno yasiyo na staha kumjibu Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu uwekezaji wa Kampuni ya DP World katika bandari ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa barua hiyo ya wito, Lissu anatakiwa kufika kwa mahojiano ili kukamilisha uchunguzi wa maneno hayo.

Kupitia ukurasa rasmi wa akaunti yake ya Twitter, Lissu ameandika hivi; “Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!