Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkutano wa uhisani Afrika kuunguruma Zanzibar
Habari Mchanganyiko

Mkutano wa uhisani Afrika kuunguruma Zanzibar

Spread the love

MKUTANO wa nane wa uhisani Afrika Mashariki (EAPC), unatarajiwa kuanza kufanyika  tarehe 28  hadi 30 Juni 2023, visiwani Zanzibar.Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 27 Juni 2023 na Afisa Mtendaji Mkuu wa EAPC, Evans Okinyi, bodi za udhamini zinazofanya hisani, taasisi na mashirika yanayofanya kazi za kijamii pamoja na yanayotoa ruzuku kwa ajili ya miradi ya maendeleo Tanzania na nchi za Afrika Mashariki, zitashiriki mkutano huo.

“Mkutano huu ni kwa ajili ya kuhamasisha suala la uhisani katika jamii na kujadili namna bora kuendeleza uhisani barani Afrika, kwa ajili ya kuleta maendeleo. Mkutano huo unaendeshwa na Mtandao wa Uhisani Afrika Mashariki (East Africa Philanthropy Network – EAPN),  kwa kushirikiana na Legal Services Facility (LSF),” imesema taarifa ya Okinyi.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki 300, ambao watabadilishana uzoefu, kufanya tathimini ya pamoja na kuunda mipango ya kihisani na kijamii ili kuwekeza katika jamii barani Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!