Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa wahisani
Habari Mchanganyiko

Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa wahisani

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng'wanakilala
Spread the love

 

TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa nane wa mtandao unaojishughulisha na masuala ya utoaji misaada kwa jamii, East African Philanthropy network (EAPN), unaotarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar Juni, 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungunza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, Afisa Mtendaji Mkuu wa EAPN, Evans Okinyi amesema mkutano huo utafanyika Zanzibar kwa siku mbili, kuanzia tarehe 28 hadi 30, Juni 2023, ambapo utajumuisha wataalam na taasisi za masuala ya uhisani zaidi ya 300.

Okinyi amesema lengo la mkutano huo ni kujadili ubunifu utakaosaidia kuhamasisha utekelezaji mipango ya uhisani pamoja na kutatua changamoto zake.

Afisa Mtendaji huyo wa EAPN, amesema mkutano huo hautanufaisha sekta ya uhisani peke yake, bali utahamasisha mabadiliko ya mifumo ili kuongeza jitihada za utoaji hisani kwa jamii.

“Haijalishi ni namna gani tunauangalia mkutano huu. Ukweli ni kwamba muingiliano wa kijamii uliopo katika ulimwengu wa sasa unahitaji jamii inayoweza kufanya kitu ama kuelewa mambo kwa namna nzuri. Tunalenga pia kuwezesha zaidi wale ambao hawawezi kusema kwa kubadilisha mitazamo yao kifikra ili kuyaangalia mambo ambayo pengine yanaonekana kuwa hayawezekani kuwa yanawezekana,” amesema Okinyi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala, amesema Shirika lake linaona fahari kuratibu mkutano huo kwa niaba ya wadau wa EAPN

“Mkutano huu ni jukwaa la kubadilishana uzoefu pamoja na kufanya tathmini ya pamoja ili kubuni njia bora za jamii kufanya hisani na kuwekeza kwa ajili jamii na wadau mbalimbali barani Afrika. Hivyo, nawaomba mashirika yote ya uhisani nchini, sekta binafsi, serikali, CSOs na wadau wengine muhimu wa maendeleo kuungana pamoja katika mkutano huu muhimu,” amesema Ng’wanakilala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!