Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia avunja bodi TRC, amtumbua bosi TGFA
Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi TRC, amtumbua bosi TGFA

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan leo  tarehe 9 Aprili 2023 ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kutengua nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.

Hatua hiyo imekuja ikiwa imepita wiki moja baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/2022. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mhandisi John Nzulule.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoyolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, Rais amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kuwaelekeza Makatibu Wakuu wa Watendaji Wakuu kusoma ripoti hiyo, kujibu na kuzifanyia kazi hoja zote.

“Watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhilifu wachukuliwe hatua za kisheria,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Ripoti ya CAG iliwasilishwa bungeni jijini Dodoma tarehe 6 Aprili 2023 na kuibua madudu yaliyofanywa na taasisi za umma ikiwamo Shirika la Reli Tanzania – TRC.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, TRC katika mwaka wa fedha 2020/2021, lilipata hasara ya Sh22.8 bilioni huku mwaka 2021/2022 ikipata hasara ya Sh31.29 bilioni.

Bodi ya Wakurugenzi ya TRC, ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti Profesa Wajanga Kondoro, Katibu wa Bodi hiyo alikuwa Masanja Kadogosa, huku wajumbe ni London Kibugula, Dk Jabir Bakari na Benjamin Mbimbi.

Wajumbe wengine ni Lilian Ngilangwa, Joseph Salema, Juma Kijavara na Peter Noni.

Aidha, ripoti hiyo ya CAG ilibainisha kuwa Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imekuwa ikipata hasara kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!