Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mpango awaasa wazazi kuwalinda watoto dhidi ya matumizi ya simu, maudhui ya katuni
Habari Mchanganyiko

Dk. Mpango awaasa wazazi kuwalinda watoto dhidi ya matumizi ya simu, maudhui ya katuni

Spread the love

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amewaasa wazazi na walezi kulea watoto wao kwa kuzingatia maadili mema ya kitanzania pamoja na kuwa makini na maudhui ya watoto (katuni) katika televisheni ili kuwaepusha na kujifunza mambo yasiofaa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Pia amewataka walimu wa shule za msingi, sekondari na hata vyuoni kukemea kwa nguvu uharibifu wa maadili ya kitanzania katika maeneo ya kutolea elimu.


Dk. Mpango ametoa kauli hiyo leo tarehe 09 Aprili 2023 alipoungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma katika Ibada ya Jumapili ya Sikukuu ya Pasaka.

Akizungumza na waumini wa Kanisa hilo mara baada ya kumalizika kwa Ibada, Dk. Mpango ambaye pia alikuwa ameambatana na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango, amewasihi wazazi na walezi kuwalinda watoto pamoja na vijana wao dhidi ya matumizi mabaya ya simu pamoja na kufuatilia mienendo yao wakati wote.

Makamu wa Rais amesema ni vema kwa wazazi kutambua marafiki wa watoto wao na kuwapa miongozo sahihi wakati wote na kutowaacha kujiongoza wenyewe.

Aidha, Makamu wa Rais amewaasa waumini na watanzania kwa ujumla kuongeza jitihada katika ulinzi na uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti katika kila kaya pamoja na usafi katika maeneo yao. Amesema ni vema wazazi kutoa mafunzo kwa watoto wao namna ya kupanda miti na kuisimamia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the love  Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya...

Habari Mchanganyiko

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk....

error: Content is protected !!