Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanajeshi 7 wahukumiwa kifo kwa kukimbia maadui
Habari Mchanganyiko

Wanajeshi 7 wahukumiwa kifo kwa kukimbia maadui

Spread the love

WANAJESHI saba wa DR Congo wamehukumiwa kifo kwa kuonyesha uoga mbele ya wapiganaji wa kikundi cha waasi wa M23 na kukimbia hali inayodaiwa kuzidisha hofu kwa wananchi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Mwendesha mashtaka wa kijeshi alisema tarehe 9 Februari 2023, wanajeshi hao walipitia katikati ya eneo la Sake, kilomita 25 magharibi mwa mji wa Goma uliopo mashariki mwa Kongo, wakipiga risasi kiholela walipokuwa wakiwakimbia waasi hao.

Hata hivyo, wanajeshi hao walikanusha mashtaka na mawakili wao walisema watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama hiyo.

Mwendesha mashtaka alisema raia wawili waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya wakati wa tukio hilo lililosababishwa na kitendo cha askari.

Maelfu ya watu hivi karibuni wamekimbia makazi yao hadi Goma na Minova huku waasi wa M23 wakikaribia mji huo kutoka eneo la Masisi magharibi.

Novemba mwaka jana, mahakama ya kijeshi ya Goma iliwahukumu kifo askari watatu kwa kukimbia vitani wakati wa makabiliano dhidi ya M23 na kusababisha hofu miongoni mwa raia.

Adhabu za kifo bado zinatolewa nchini DR Congo lakini mara ya mwisho zilitekelezwa mwaka 2003. Aidha, adhabu hizo zimeanza kubadilishwa taratibu na kuwa kifungo cha maisha.

1 Comment

  • Nawapa pole sana maskari hao kwa hukumu hiyo iliyotolewa,japo wamekiuka kiapo chao ila badala ya kifo basi wahukumiwe kifungo cha maisha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Elimu ya utunzaji wa mazingira ipewe kipaumbele kwa watoto

Spread the love  JAMII imetakiwa kuwajengea Watoto tabia ya utunzaji wa mazingira...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

error: Content is protected !!