Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kauli ya Mwigulu yatibua Bunge, Spika aifuta
Habari za SiasaTangulizi

Kauli ya Mwigulu yatibua Bunge, Spika aifuta

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson
Spread the love

 

KAULI ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba aliyoitoa bungeni kuwa “wabunge wajadili mambo mengine yanayohusu uganga” imeendelea kuutibua muhimili huo kwa zaidi ya wiki moja na sasa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson, ameifuta rasmi kwenye taarifa rasmi za Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Spika amefuta kauli hiyo leo Alhamisi tarehe 9 Februari 2023 wakati akitoa mwongozo ulioombwa na Dk. Mwigulu baada ya Mbunge wa Tandahimba, Ahmed Katani, kumtuhumu kuwa amewatukana wabunge na kumtaka ajitafakari.

Kwa mujibu wa Spika Tulia, mwongozo uliiombwa na Dk. Mwigulu unaeleza kuwa kauli iliyotolewa na Katani kuwa amewatukana wabunge ni uongo na hivyo kutaka mwongozo wa spika kuhusu kauli hiyo.

Kutokana na hali hiyo Spika amesema amelazimika kupitia taarifa za bunge na kujiridhisha kuwa wabunge wamekuwa wakirejea kauli ya Dk. Mwigulu kwa namna hasi kuonesha kutoridhishwa nayo.

Aidha amesema amejiridhisha kuwa chanzo cha malalamiko ya wabunge ni kauli aliyoitoa Dk. Mwigulu ambayo amesema haikuwa na staha.

Sasa baada ya kuzipitia taarifa rasmi za bunge ni Dhahiri kwamba maneno hayo Mheshimiwa Mwigulu aliyasema,” amesema Spika.

Amesema kwamba kwa mujibu wa Kanuni hasa masharti yaliyowekwa chini ya kanuni ya 71 yanataka matumizi ya lugha ya staha bungeni.

“Uamuzi sasa wa kiti kwasababu haikuombwa mwongozi ulikuwa umeombwa utaratibu kujua kama kanuni imekiukwa au Hapana, lakini kwasabbau maneno haya yameendelea kujadiliwa hapa bungeni na ili sasa lifike mwisho haya maneno yaliyosemwa na Dk. Mwigulu kwamba ‘hebu tujadili mambo mengine huko yanayohusu uganga wa kienyeji na vitu vingine kwenye uchumi this is my professional’ yafutwe kwenye taarifa rasmi za bunge,” amesema Dk. Tulia.

Hata hivyo Spika amewataka Wabunge kufuata kanuni na kujikita katika kuchangia hoja badala ya kushughulika na mtu halikadhalika mawaziri wanapojibu wajikite kwenye hoja badala ya kumjibu mtu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!