Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi mbaroni tuhuma za rushwa ya Sh milioni 100
Habari Mchanganyiko

Polisi mbaroni tuhuma za rushwa ya Sh milioni 100

RPC Arusha, Justine Masejo
Spread the love

MMOJA  wa askari anayetuhumiwa kuhusika na tukio la kuomba rushwa ya Sh milioni 100 kwa mfanyabiashara wa Usa River Jijini Arusha, Profesa Justine Maeda na kutoroka na ushahidi wa meno ya tembo, anashikiliwa katika kituo cha Polisi, Usa River. Anaripoti Joseph Ngilisho, Arusha…(endelea).

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Afrusha, Justine Masejo amethibitisha kukamatwa kwa Konstebo Zakhayo na kuongeza kuwa jalada la kesi hiyo linashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa.

‘’Ni kweli, Konstebo Zakhayo amekamatwa ila kesi hiyo ni ya TAKUKURU ni vema ukawauliza wanaweza kujua, sisi tumetimiza wajibu wa kukamata kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akitafutwa muda mrefu, baada ya kufanya tukio hilo alitoroka chini ya ulinzi wa Polisi,’’ alisema Kamanda Masejo.

Habari kutoka vyanzo vya ndani ya Polisi Usa River, zilisema Konstebo Zakhayo alikamatwa Kijenge Juu kata ya Kimandolu jijini hapa nyumbani kwa mkewe alikorudi kujificha baada ya kutokomea mafichoni kusikojulikana.

Konstebo Zakhayo na askari wenzake saba wakiwamo watano wa kituo cha Polisi Usa River na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha na raia watatu wa Usa River, walikamatwa na taarifa ambazo gazeti la Raia mwema linazo, zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi mwaka jana.

Askari waliokamatwa (majina yanahifadhiwa) ni wakaguzi wasaidizi wawili, koplo na makonstebo wanne; wawili wa kituo kikuu waliotoroka lindo na kwenda kufanya uhalifu wakiwa na silaha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!