Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko India kushirikiana na Tanzania kuongeza thamani madini
Habari Mchanganyiko

India kushirikiana na Tanzania kuongeza thamani madini

Spread the love

SERIKALI ya India imeahidi kushirikiana na Tanzania katika uendelezaji wa teknolojia za uongezaji thamani madini nchini kupitia Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Hayo yamebainishwa na Waziri anayeshughulikia Migodi nchini India, Pralhad Joshi wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko katika ofisi za Waziri huyo nchini India.

Josh amesema Serikali ya India imeonesha nia ya kuwekeza nchini katika madini ya Kimkakati na makaa ya mawe.

Kutokana na uwepo wa fursa hizo Dk. Biteko na Waziri wa India wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika Sekta ya Madini kati ya Tanzania na India.

Pia, aliahidi kuendeleza ushirikiano kupitia Wizara ya Biashara ya nchini India na Baraza la kukuza usafirishaji vto na bidhaa za usonara ( Gem and Jewellery Export Promotion Council).

Katika hatua nyingine, Waziri wa Madini Dk. Biteko alikutana na Kampuni ya Cancastmaxx katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini India ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika makaa ya mawe nchini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Dk. Biteko aliiagiza kampuni hiyo kufuata taratibu na kujiridhisha ili kutimiza azma ya kuwekeza Tanzania.

Pia, Dk. Biteko alikutana na na wadau wa Baraza la kukuza Usafishaji vito na bidhaa za usonara kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye tasnia ya uongezaji thamani madini na kutangaza fursa zilizopo katika tasnia ya madini.

Wadau hao walikubali kushurikiana katika kuboresha tasnia ya uongezaji thamani madini nchini kupitia Kituo cha TGC na kukuza masoko ya madini ya vito.

Dk. Biteko alitembelea Kiwanda cha kukata na kung’arisha madini ya vito na utengenezaji wa bidhaa za usonara ambapo alishuhudia ukataji wa madini ya vito na utengenezaji wa bidhaa za usonara zenye ubora wa kiwango cha juu.

Katika ziara hiyo, Dk. Biteko aliambatana na Kamishna wa Madini Dk. Abdulrahman Mwanga, Mwenyekiti wa Bodi ya TGC Dk. George Mofulu na Mratibu wa TGC Daniel Kidesheni na wakufunzi kutoka kituo hicho Jumanne Shimba, Ester Njiwa na Cleophas Siame.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!