Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aonya wanasiasa wanaotetea wavamizi wa ardhi kisa kura
Habari za Siasa

Rais Samia aonya wanasiasa wanaotetea wavamizi wa ardhi kisa kura

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wanasiasa kuacha kuchochea migogoro ya ardhi kwa kutetea wavamizi wa ardhi kwa malengo ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Amesema wanasiasa hukaa kimya wakati maeneo hayo yanapovamiwa lakini baadae husimama na kuwatetea ili tu kupata kura wakati wa uchaguzi.

Mkuu huyo wa nchi amewaonya kuacha kusimama na kutetea wavamizi wa mazingira na kuharibu mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Rais Samia ametoa onyo hilo leo Jumatano tarehe 23, Novemba, 2022 akiwa ziarani mkoani Manyara kuelekea mkoani Arusha.

“Unajua kwamba wamevamia na wameharibu mipango ya matumizi bora ya ardhi, unasimama kuwatetea ili upate kura,” amesema Rais Samia.

Kutokana na hali hiyo amewaomba wanasiasa wasimame na Serikali katika kupanda matumizi bora ya ardhi ili wananchi waweze kupata maeneo ya kufanyia shiughuli zao.

“Wanasiasa simameni na Serikali yenu tupange matumizi bora ya ardhi kila mwananchi apate maeneo ya kutumia anayefuga afuge lakini tusichochee kwenda kuvamia maeneo ambayo hayakupangwa kwa matumiz hayo ambayo wamejiamulia,” amesisitiza Rais Samia.

Amewasihi wasichochee migogoro kwani inapoteza muda mwingi na kuchelewesha maendeleo.

“Eneo ambalo wananchi wangelitumia kwa maendeleo halitumiki kwasababu lipo kwenye mgogoro hadi umalizike. Niombe sana wananasiasa tusaidiane kwenye jambo hili tusichochee migogoro,” amesema

Aidha Rais Samia ameeleza kushuhudiwa kwa mwenendo mbaya wa unyeshaji wa mvua huku kukiwa na vipindi virefu vya jua unaotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo amebainisha kusababishw ana uharibifu wa mazingira.

Amewahimiza wananchi kutunza mazingira na kupanda miti ili mazingira yarudi na kusaidia kupatikana kwa maji na mvua za kutosha.

Amesema pia mabadiliko hayo yamesababisha maziwa na bahari kujaa na kuingilia makazi ya watu.

Amesema mwaka jana ilishuhudiwa kipindi kirefu cha jua na kusababisha vifo vya mifugo hasa katika mkoa huo wa Manyara.

“Yote ni kwasababu tunaharibu mazingira, niombe sana twende tukashughulikie tena mazingira yetu ili tuweze kuwa na vipindi vya kutabirika,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!