RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi kuendeleza juhudi katika kilimo kwani Seerikali imechukua hatua za kukuza kilimo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).
Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 23, Novemba, 2022, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Manyara amabo ameutaja kama miongoni mwa mikoa inayotegemewa kwa kilimo nchini.
Rais Samia amesema uzalishaji wa chakula kwa mwaka 2021 ndani ya mkoa wa Manyara ulizalisha ziada ya tani 264,819 ambazo ziliuzwa nje ya mkoa.
“Sasa mkiongeza jitihada zaidi mtazalisha zaidi ya hizi na nasema hivi kwasababu tumeanza kujenga maghala na vihenge ambavyo vinakwenda kuchukua tani nyingi za chakula,” amesema.
Amesema anahimiza kilimo kwasababu miaka ijayo dunia itakuwa na hatari ya njaa na kwamba Tanzania haina sababu ya kulia njaa.
Amesema wanachukua hatua kwa kuweka miundombinu ya mbolea, umwagiliaji, kuanza kilimo cha mashamba makubwa ili chakula kiwe kingi cha kuweka akiba na kuuza kwa majirani.
“Tanzania Mungu ametupendelea ardhi, nzuri, maji tunayo, mvua zinanyesha kwa wakati wake la maana ni kkinga maji na kuyahidhi yatumike kwenye kilimo na matumizi mengine,” amesema Rais Samia.
Leave a comment