Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko PSSSF: Waajiri wanasababishia tozo kwa mafao ya wastaafu
Habari Mchanganyiko

PSSSF: Waajiri wanasababishia tozo kwa mafao ya wastaafu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako
Spread the love

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeweka wazi kuwa kitendo cha waajiri kuchelewesha michango ya watumishi kinasababisha tozo ya ucheleweshaji wakati wa kulipa mafao kwa wanachama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Akizungumza jana tarehe 6 Novemba 2022, jijini Dar es Salaam, wakati wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC), Meneja wa PSSSF Temeke, Rajabu Kinande amesema kitendo cha mwajiri kuchelewesha mchango huo kunaathiri mafao ya mwanachama.

“Ili kupunguza malalamiko ni vyema waajiri kutimiza wajibu wao kisheria wa kulipa michango ya watumishi wake ndani ya mwezi mmoja baada ya mwisho wa mwezi husika” alisema Kinande.

Kinande alisema utaratibu wa kufanya malipo upo kiteknolojia ambapo kumbukumbu za malipo zitahifadhiwa.

Kwa sasa mwajiri ana uwezo wa kutengeneza namba za kumbukumbu ya malipo itakayomuwezesha kulipa michango na kupata risiti kupitia mtandao,” alieleza.

Wakati huo huo Kinande alisema wastaafu wengi wanachelewa kupata mafao yao kutokana na kuchelewesha taarifa zao za kustaafu kabla ya miezi sita.

Aidha, alisema kuwa hakuna watumishi wanaowafanyia mpango wastaafu wengine kupata mafao mapema badala yake uwahishaji wa taarifa zao ndio unawasaidia kupata stahiki zao haraka.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo, mtumishi anatakiwa kuanza kufuatilia mafao yake kwa kupeleka taarifa zote muhimu katika ofisi hizo ili zianze kufanyiwa kazi ikiwemo kufuatilia kama waajiri wamechangia miezi yote kama inavyotakiwa na sheria.

Alisema kila mwaka mfuko huo hufanya uhakiki wa wastaafu na wategemezi wanaopata pensheni kwa lengo la kusafisha daftari la wastaafu na kuhakikisha pensheni inalipwa kwa walengwa na si vinginevyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!