Monday , 20 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makonda apewa siku 14 kujitetea shitaka la kukwapua Range Rover
Habari za SiasaTangulizi

Makonda apewa siku 14 kujitetea shitaka la kukwapua Range Rover

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa siku 14 kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwasilisha majibu yake dhidi ya kesi ya madai aliyofunguliwa na mfanyabiashara Patrick Kamwelwe. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amri hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate, wakati kesi ilipotajwa kwa mara ya kwanza.

Hakimu Kabate alitoa amri hiyo baada ya Wakili Gift Joshua anayemwakilisha Paul Makonda ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo Na. 234/2022, kudai kuwa mteja wake hajapata hati ya madai.

Kufuatia madai hayo, Hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 8 Novemba 2022, ambapo itatajwa tena.

Kamwelwe amefungua kesi hiyo ya madai, akiiomba mahakama imuamuru Makonda na mwenzake, William Malecela maarufu kama Le Mutuz, wamlipe zaidi ya Sh. 247.2 milioni, kama fidia ya kupora gari lake aina ya Range Rover.

Kamwelwe anadai kuwa Makonda kupitia kwa Le Mutuz, alimuazima gari hilo kwa ajili ya kulitumia kwa muda wa wiki mbili, kisha alirudishe lakini hadi sasa hajarudishiwa gari lake.

Katika kesi hiyo, Kamwelwe anaiomba mahakama  imuamuru Makonda na mwenzake, kumlipa kiasi hicho cha fedha kama fidia anayodai kuwa, imetokana na hatua ya wadaiwa hao kumdhulumu gari lake jeusi aina ya Toyota Land Rover/Range Rover Sport, yenye namba za chesis 20153.

Katika mchanganuo wa fedha hizo, Sh. 247,243,750, ambazo ni sawa na dola za Marekani 106,250, Kamwelwe anamtaka Makonda na mwenzake, walimpe dola 11,250, kama gharama ya kodi ya kuliingiza gari hilo. Dola 50,000, fidia ya kutwaa gari, pamoja na dola 45,000, ambayo ni thamani ya gari.

Patrick Kamwelwe

Kamwelwe ambaye pia anajulikana kwa jina maarufu kama PCK amedai Makonda ameendelea kuitumia gari hiyo hata baada ya kuondolewa madarakani licha ya kwamba si mali yake halali.

Kamwelwe ambaye ni mzaliwa wa Mpanda – Rukwa aliyekuwa akiishi jijini Dar es Salaam kabla ya kukimbilia Marekani kutokana na vitisho, amedai kwamba baada ya kufuatilia ili arejeshewe gari hiyo ndipo vitimbi vilipoanza na kubambikiwa kesi ya jinai ya kumiliki mali haramu.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni alisema kutokana na tuhuma hizo Juni 2017 alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akaunti zake za benki pamoja na mali zake zikishikiliwa mpaka sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!