Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TPA yajipanga kuiondoa nchi katika uchumi wa tatu kwenda wa pili
Habari MchanganyikoTangulizi

TPA yajipanga kuiondoa nchi katika uchumi wa tatu kwenda wa pili

Mkurugenzi Mkuu, Plasduce Mbossa
Spread the love

 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imedhamiria kufanikisha maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufanya mageuzi makubwa ya uchumi wa nchi kutoka daraja la tatu kwenda kwenye nchi zenye uchumi wa daraja la pili. Anaripoti Erasto Masalu, Pwani … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu, Plasduce Mbossa alipokutana na Wahariri kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari katika kikao kazi kilichofanyika Bagamoyo Mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa TPA.

Mkurugenzi Mkuu Mbossa amesema kuwa TPA inajipanga kuzifikisha bandari zake katika kiwango cha juu na cha kisasa kwa kuziunganisha na shughuli za biashara ya kitaifa na kimataifa.

“Bandari zenye uwezo mdogo na ufanisi wa chini ni kikwazo kikubwa katika shughuli za uzalishaji na biashara ambacho kinaongeza gharama za huduma za bandari ambazo zinaishia kulipwa na walaji ambao ni wananchi wa kawaida wakati wa kununua huduma na mahitaji yao ya kila siku.

“Katika hili bandari hazipaswi kuwa na gharama kubwa za utoaji wa huduma zake kwa sababu haijapewa jukumu la kisheria la kukusanya mapato kuwa na bandari zenye ufanisi na manufaa kwa mwananchi mmoja mmoja na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu, Plasduce Mbossa (hayupo pichani)

Amesema TPA iko tayari kuhakikisha dira ya Serikali inatekelezwa kwani itakuwa ni hatua muhimu katika kuzifikia nchi zenye uchumi wa daraja la kwanza.

Mbossa amesema kuwa kipimo cha maendeleo ya bandari zetu nchini ni bandari za mwambo wa Pwani hususan bandari ya Dar es Salaam ambayo imekuwa tegemeo la nchi yetu na nchi jirani za Zambia,JaMhuri ya kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Malawi na Uganda.

“Pamoja na kuwa tegemeo letu, bado kuna maboresho ya miundombinu na ya kiutendaji yanayopaswa kufanyika katika bandari zetu zote ili ziweze kuwa lango la biashara ya kitaifa na kimataifa” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa hivi sasa Serikali ya Awamu ya Sita, inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uboreshaji wa bandari na ujenzi wa bandari mpya ili kuongeza uwezi kabla ya mahitaji.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu, Plasduce Mbossa (hayupo pichani)

Mbossa amesema kuwa kupitia maboresho yanayoendelea kutekelezwa , uwezo kuhudumia shehena katika bandari za Dar es Sakaam, Tanga na Mtwara unatarajiwa kufikia jumla ya tani milioni 27.5 ifikapo mwaka 2024/25 wakati matarajio ya shehena ni jumla tani milioni 26.1 ifikapo mwaka huo sawa na asilimia 94.9 ya uwezo wa bandari zetu za mwambao utakaokuwepo.

“Kutokana na matarajio ya shehena kuwa karibu na uwezo wa juu wa bandari zetu, tunapaswa kuanza kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa bandari za Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani, Chongoleani katika Mkoa wa Tanga na Kisiwa-Mgao katika Mkoa wa Mtwara ili kuongeza uwezo wa bandari zetu.

“Vilevile kwa upande wa bandari za maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa, tumeboresha bandari zilizokuwepo na kujenga zingine mpya ikiwa ni pamoja na bandari ya Nyamirembe, Lushamba, Ntama za ziwa Victoria, Karena na Kagunga za ziwa Tanganyika na tumefanya maboresho ya bandari za Kiwira na Itungi za ziwa Nyasa,’ amesema.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu, Plasduce Mbossa (hayupo pichani)

Amesema kuwa Serikali kupitia mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), imekamilisha mpango kabambe wa uendelezaji wa bandari za Tanzania kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi 2045 kwa lengo la kuziboresha ili kuendana na matarajio ya ongezeko la shehena na kufikia ufanisi unaotakiwa.

“Serikali inatakiwa kuwekeza katika miundombibu, ununuzi wa mitambo, mifumo ya uendeshaji wa bandari, kuboresha uendelezaji, usimami na uendeshaji wa bandari,” amesema.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!