Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadhamini NMB Marathon watambulishwa rasmi
Habari Mchanganyiko

Wadhamini NMB Marathon watambulishwa rasmi

Spread the love

WIKI moja kabla ya kufanyika ya mbio za hisani za NMB Marathon ‘Mwendo wa Upendo,’ Benki ya NMB inayoandaa mbio hizo imetangaza wadhamini zaidi ya 20 ambao wameeleza siri ya uamuzi wa kukubali kudhamini kuwa ni kuguswa na wazo chanya la benki hiyo kuwakomboa kinamama nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza wakati wa utambulisho huo jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori, aliwashukuru wadhamini hao kwa kusapoti mbio hizo na kurahisisha lengo lengo la kukusanya Sh. Mil. 600 mwaka huu, hivyo kutoa nafasi mapato ya miaka miwili ijayo ya mbio hizo kuyaelekeza katika maeneo mengine yenye uhitaji.

 

Aidha, aliwataja wadhamini wakuu wa kuwa ni Sanlam Life Insurance na UAP Insurance (Executive), huku Jubilee General Insurance (ikiwa kategori ya Gold).

Wadhamini wa kundi la Bronze ni pamoja na Alliance Life Assurance, Britam Insurance Tanzania, Reliance Insurance, ARiS Risk and Insurance Solutions na Metropolitan Life Insurance.

Wengine wa kundi hilo ni pamoja na, huku Toyota, TBL, Strategis, Serena Hotel, Azam, na Johari Rotana Hotel wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wengineo.

Katika kundi la vyombo vya habari washirika, Kimori aliitaja EFM Radio, TV E, Mwananchi Communications Limited, IPP Media na Almasi Productions, orodha ilikamilishwa na Kampuni za SGA Security Tanzania, Gelato na Grano Coffee.

Lakini pia, wadhamini hao waliipongeza NMB kwa wazo chanya la kulikomboa kundi la kinamama wanaoshindwa kujitibu fistula kutokana na gharama kubwa na kwamba kujitokeza kwao kuunga mkono jambo hilo, ni uthibitisho kwamba afya ya mama ni kipaumbele muhimu kwa jamii.

NMB Marathon 2022, zinazolenga kukusanya kiasi cha Sh. milioni 600 za kusaidia matibabu ya kina mama wenye matatizo la fistula wanaotibiwa kwenye Hospitali ya CCBRT, zitafanyika Oktoba 1 kwenye viwanja vya Leaders Club huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

error: Content is protected !!