Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu mwingine Anglikana afariki dunia, Dk. Mwinyi amlilia
Habari Mchanganyiko

Askofu mwingine Anglikana afariki dunia, Dk. Mwinyi amlilia

Askofu John Ackland Ramadhani
Spread the love

 

ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, John Ackland Ramadhani amefariki dunia jana tarehe 12 Septemba, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea).

Askofu Ramadhani amekuwa askofu wa pili kupoteza maisha katika kipindi cha wiki mbili kwani tarehe 3 Septemba mwaka huu, Askofu George Chiteto wa Kanisa Anglikana dayosisi ya Mpwapwa alifariki baada ya kumaliza kuhubiri katika misa ya mazishi ya mke wa askofu mwenzake Hilda Lugendo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 12 Septemba, 2022 na Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mwinjilisti Canon Bethuel Mlula imeeleza kuwa, Mhashimu Baba Askofu Mkuu, Kanisa Anglikana Tanzania, Maimbo William Mndolwa amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Askofu Ramadhani.

Askofu, alizaliwa huko Zanzibar tarehe 1 Agosti, 1932 akiwa ni mtoto wa Metthew Douglas Ramadhani na Bridget Ann Constance Masoud.

Alihitimu shahada katika chuo kikuu cha Afrika Mashariki na baadae chuo cha Queens, Birmingham na chuo kikuu Birmingham cha nchini Uingereza.

Aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha Ualimu cha St. Andrews, Korogwe kuanzia 1967 hadi 1969. Alipata daraja la Ukasisi mwaka 1976 huko Zanzibar. Alikuwa Mkuu wa chuo cha Theolojia cha St. Mark’s, jijini Dar es salaam, kuanzia mwaka 1977 hadi 1979.

Aliwekwa wakfu kuwa Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar na Tanga katika kanisa la Mtakatifu Augustino, Chumbageni, tarehe 27 Januari,1980 akimfuatia baba Askofu Yohana Jumaa, (1968-1980).
John Ramadhan alikuwa Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar na Tanga hadi mwaka 2001- 2002 kabla ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Douglas Matthew Toto (2002-2006).

Aliwekwa kwa kitini kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana mwaka 1984 na alihudumu hadi mwaka 1998 alipostaafu na kufuatiwa na Askofu Donald Leo Mtetemela (1998-2008).

Kabla ya kuwa Askofu wa kanisa la Anglikana, John Ramadhani, alikuwa Mhadiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

“Ndani ya Kanisa la Anglikana Tanzania, John amehudumu katika nyadhifa mbalimbali na amehusika kutoa mchango mkubwa kwa kanisa na jamii. Kanisa tutaendelea kuyaenzi mema yote aliyoyafanya baba Askofu kipindi cha uhai wake.

“Tunatoa pole kwa familia ya baba Askofu , wahudumu na Wakristo wote wa Dayosisi ya Zanzibar na Kanisa lote kwa ujumla kwa msiba huu mkubwa . Taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana na familia. Amani ya Mungu, ipitayo akili zote, iwahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika kristo Yesu,” imeeleza taarifa hiyo.

Wakati huohuo, Rais wa Zanzibar. Dk. Hussein Ali Mwinyi leo tarehe 13 Septemba, 2022 ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na wakristo wa Kanisa la Anglikana Tanzania kutokana na kifo hicho.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hillary imeeleza kuwa: “Rais Dk. Mwinyi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Baba Askofu Ramadhani. Askofu atakumbukwa kwa busara, upole na unyenyekevu uliotukuka na kiongozi aliyetamani kuona kanisa linakua chini ya misingi ya Amani.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!