Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watanzania wahimizwa kutumia bidhaa zenye nembo ya TBS
Habari Mchanganyiko

Watanzania wahimizwa kutumia bidhaa zenye nembo ya TBS

Spread the love

MENEJA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya kati, Nickonia Mwambuka amewataka watanzania kuhakikisha wanatumia bidhaa zenye nembo ya TBS kwa nia ya kulinda afya zao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Amesema ni muhimu jamii ikatambua matumizi bora ya bidhaa zenye viwango ili kuepukana na madhara ambayo yanaweza kujitokeza pale ambapo watatumia bidhaa ambazo hazina viwango na kuthibitishwa na Shirika husika.

Mwambuka ametoa kauli hiyo leo tarehe 7 Agosti, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Dk. Paskas Mragiri katika banda la shirika hilo katika viwanja vya maonesho vilivyopo Nzuguni Nanenane Jijini hapa.

Amesema alama hiyo ni uthibitisho kwa mzalishaji na mlaji kuwa bidhaa husika ni bora na salama kwa matumizi na Mazingira.

Aidha, amesema alama ya ubora ya TBS huwafanya wanunuzi kununua bidhaa na kutumia bila wasiwasi wowote.

“Kwa upande mwengine alama hiyo humlinda mzalishaji katika ushindani dhidi ya bidhaa hafifu na kumuwezesha kulihakikishia soko lake kuwa  bidhaa yake inakidhi matakwa yaliyobainiswa Katika kiwango na hivyo ni bora na Salama kwa matumizi yaliyokusudiwa.

“TBS ina skimu mbili za udhibiti ubora mojawapo ya skimu hizo ni skimu ya alama ya ubora ambapo chini ya skimu hii mzalishaji ambaye bidhaa yake imethibitishwa ubora kwa kuzingatia kiwango cha kitaifa cha bidhaa husika hupewa leseni ya kutumia alama ya TBS Katika bidhaa hiyo,” amesema Mwambuka.

Hata hivyo, alipoulizwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Paskas Mragiri juu ya bidhaa bandia zinazosafirishwa kutoka mikoa na nchi mbalimbali Meneja huyo amesema  wamekuwa wakifanya kaguzi za mara kwa mara na wamekuwa wakikamata na kutelekeza bidhaa hizo bandia.

Hata hivyo, amesema  Shirika limetenga kiasi cha Sh. milioni 581 kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uthibitishaji wa mifumo ya kiutendaji.

Amesema kwa sasa TBS imepatiwa ithibati ya kufanya shughuli hiyo na mashirika yanaweza kuthibitishiwa ubora wa mifumo yao ya kiutendaji kupitia TBS jambo ambalo linazidi kuwahakikisha wananchi wanapokea huduma zilizo bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!