Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia: Mwelekeo wa elimu yetu ni kuwapa vijana ujuzi
Habari MchanganyikoTangulizi

Samia: Mwelekeo wa elimu yetu ni kuwapa vijana ujuzi

Spread the love

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema maboresho ya Miundombinu yanayoendelea katika sekta ya elimu yanalenga kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu inayowapatia ujuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza leo tarehe 7 Agosti, 2022 baada ya kuzindua miundombinu iliyojengwa na kukarabatiwa na Serikali kwa kushirikiana na serikali ya Canda kupitia Mradi wa Kuboresha Vyuo vya Ualimu Nchini, amesema ukarabati huo utakwenda sambamba na uboreshaji wa mitaala pamoja na mapitio ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ukarabati na uboreshaji wa miundombinu katika Vyuo vya Ualimu ni sehemu ya mikakati ya Wizara  ya kuleta mageuzi katika sekta kwa kuhakikisha elimu inatoa ujuzi ili kuandaa wahitimu wanaoendana na soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa Wizara inakamilisha Rasimu za Sera na Mitaala ya Elimu Msingi na kwamba Wizara itakuwa na  kongamano kubwa litakalofanyika Mwezi Oktoba la kupokea maoni kutoka kwa wadau juu ya rasimu ya Mitaala na ya  Marekebisho ya Sera ya Mwaka 2014.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!