Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 37 zatumika kiwanja cha ndege cha Songea
Habari Mchanganyiko

Bilioni 37 zatumika kiwanja cha ndege cha Songea

Spread the love

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete kukamilika kwa upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea uliogharimu takribani shilingi bilioni 37 kutawezesha ndege sita za kubeba abiria takribani 70 kuhudumiwa kwa wakati mmoja kwa saa 24 siku saba za wiki.  Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza mkoani Ruvuma mara baada ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho, Naibu Waziri huyo amesema Serikali iliangalia fursa zilizopo mkoani humo ikiwemo uchimbaji wa Makaa ya Mawe, Utalii, Kilimo na kuamua kuboresha kiwanja hicho ili kurahisisha biashara na shughuli za usafirishaji na uchukuzi.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Ephatar Mlavi kuhusu maendeleo ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha SOngea, wakati Naibu Waziri huyo alipokagua maendeleo yake Mkoani Ruvuma.

“Mkoa huu una fursa nyingi hivyo kama Serikali tukaona tuboreshe kiwanja hiki ili wafanya biashara, wawekezaji na wananchi waweze kuwa na urahisi wa usafiri kwani biashara huwa hazina mipaka zinaweza kufanyika saa 24″, amesema Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete, amewataka Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwa na maono ya kuboresha kiwanja hicho kufikia kuhudumia ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 300.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete amewapongea TANROADS na TAA kwa kuhakikisha mkandarasi anazingatia thamani ya fedha na viwango kwenye ujenzi wa kiwanja kwa kumsimamia kwa karibu.

Naye, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma, Eng. Ephatar Mlavi, amesema kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 90 na kazi zinazoendelea ni pamoja na kukamilisha jengo la muda la kuongozea ndege na usimikaji wa taa kwenye barabara ya kuruka na kutua ndege.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la muda la kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Songea, mkoani Ruvuma. Jengo hilo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa kiwanja hicho ambao umegharimu kiasi cha shilingi takribani bilioni 37 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu.

Mhandisi Mlavi ameongeza kuwa kiwanja hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Agosti ambapo mkandarasi anatarajia kukikabidhi kazi zote mwezi Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songea, Jafari Mbana, amesema kukamilika kwa upanuzi huo kumeongeza safari za ndege hususani kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwani imeongeza safari zake kutoka safari mbili mpaka tatu kwa wiki.

Upanuzi wa Kiwanja cha ndege cha Songea  umehusisha barabara ya kuruka na kutua ndege kutoka mita 1625 hadi mita 1860 na upana mita 30, ujenzi wa uzio, jengo la muda la kuongozea ndege, maegesho ya ndege, taa, gari la zimamoto na mifumo mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!